Waziri wa mambo ya ndani wa Sudan Bw. Khalil Pasha Sairin amesema, jumla ya watu 68 wamefariki kuanzia mwezi Juni mwaka huu kutokana na mvua kali na mafuriko yaliyozikumba sehemu nyingi nchini humo.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana, Bw. Sairin amesema, serikali ya Sudan itatuma ujumbe wa ngazi ya juu kufanya uratibu kwenye sehemu zilizokumbwa na maafa, ambao utajumuisha Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Utabiri wa Hewa,na kutoa msaada wa lazima kwa sehemu hizo.