Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha mkutano wa dharura kujadili hali ya wasiwasi katika Ukanda wa Gaza, kutokana na ombi lililotolewa na Algeria.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya siasa na ulinzi wa amani Bibi Rosemary DiCarlo, na mkuu wa idara ya kuchangisha fedha kwa ajili ya misaada ya kibinadamu katika Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja huo Bi. Lisa Doughten walitoa ripoti kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza.
Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong amesema, China inasisitiza tena kuwa jambo muhimu ni kutimiza mara moja usitishwaji vita wa kudumu kwa pande zote huko Gaza, ili kuepuka hali kuwa mbaya zaidi. Amesema China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kupunguza maafa ya kibinadamu, kutekeleza “Mpango wa Nchi Mbili”, na kutimiza utulivu na usalama wa kudumu huko Mashariki ya Kati.