Algeria yasafirisha mafuta kwenda Lebanon kuisaidia kupunguza uhaba wa nishati
2024-08-19 08:15:54| CRI

Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria ameamuru usafirishaji wa haraka wa mafuta kwenda Lebanon, ambayo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nishati.

Uamuzi huo uliwasilishwa na waziri mkuu wa Algeria Bw. Nadir Larbaoui kwa mwenzake wa Lebanon Bw. Najib Mikati.

Bw. Larbaoui amemhakikishia Bw. Mikati kuwa usafirishaji huo unaakisi ahadi ya Algeria ya kuiunga mkono Lebanon katika nyakati hizi za changamoto, ili kuisaidia nchi hiyo kurejesha gridi yake ya taifa.

Gridi ya taifa la Lebanon ilikatika baada ya kituo cha mwisho cha umeme kuishiwa na mafuta, hali inayovuruga utendaji wa miundombinu muhimu kote nchini humo, ikiwemo viwanja vya ndege, bandari, pampu za maji, mifumo ya maji taka na magereza.