Kenya imeandaa kongamano la kuhimiza matumizi ya Dawa za Jadi za China (TCM) barani Afrika.
Akizungumza kwenye kongamano hilo la kimataifa la siku moja kuhusu Ushirikiano kati ya China na Afrika kwa Afya ya Wanawake na Watoto, mkurugenzi katika Idara ya Matibabu jumuishi ya Kichina na kimagharibi katika Hospitali ya Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto ya Mkoa wa Hunan, Liang Huizhen, amesema kuna ufanano kati ya Dawa za jadi za China na dawa za Afrika, akibainisha mbinu za jumla badala ya kuzingatia tu kubainisha magonjwa.
Amesema Dawa za jadi za China zina manufaa mengi , ikiwa ni pamoja na matumizi ya mitishamba ya asili ya kutibu magonjwa, na kwamba nia ya China ni kupanua ushirikiano na Afrika ili kuimarisha matumizi ya Dawa za jadi za China kuboresha matokeo ya afya katika bara zima la Afrika.