Zaidi ya watu 100 wahofiwa kupotea baada ya boti kuzama magharibi mwa DRC
2024-08-21 10:40:08| CRI

Zaidi ya watu 100 wanahofiwa kupotea baada ya boti kuzama Jumapili Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), vyombo vya habari vya ndani viliripoti Jumanne.

Kwa mujibu wa maafisa wa eneo hilo, boti hiyo ilizama mwendo wa saa moja usiku, kwa saa za huko, kwenye Mto Lukenie, Mkoa wa Mai-Ndombe, baada ya kugonga vipande vya mbao chini ya maji, ikiwa na takriban watu 300.

Watu chache tu wamenusurika, na miili kadhaa imepatikana, zilisema ripoti za vyombo vya habari vya ndani, zikiwakariri maafisa ambao walidai "ni vigumu kufafanua juu ya idadi ya majeruhi."

Gavana wa Mai-Ndombe Nkoso Kevani Lebon, alisema amesikitishwa na majali hiyo, na kuahidi kwamba watafanya uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini hatua za kuchukua.