Watu 30 waliokamatwa Jumatatu usiku kwa kukojoa na kutupa takataka katika mitaa ya Nairobi wamehukumiwa kutumikia jamii ikiwemo kusafisha chumba cha kuhifadhia maiti na kufagia mitaa iliyochaguliwa katika Wilaya Kuu ya Biashara (CBD). Waliobaki waliamriwa kusafisha bustani ya Uhuru Park.
Geoffrey Mosiria, afisa mkuu mazingira, aliyeongoza operesheni hiyo alisema hili litakuwa fundisho kwa wengine: Ukikutwa unachafua jiji, utakamatwa, utafikishwa mahakamani na kuhukumiwa, akitumai kuwa waliokamatwa watakuwa mabalozi ambao wataonya wengine dhidi ya kurudia kosa hilo.