Kongamano la siku moja kuhusu ujumuishwaji wa kifedha wa kidijitali kati ya China na Afrika limewaleta pamoja washiriki zaidi ya 100, wakiwemo maofisa kutoka benki kuu na serikali, na maofisa kutoka taasisi za kifedha za maendeleo za China na Afrika, na kujadili jinsi ya kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha.
Ofisa mkuu wa uwekezaji kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Grace Kyokunda amesema Afrika inaweza kujifunza uzoefu wa China wa kutimiza ujumuishwaji wa kifedha kupitia teknolojia za simu za mkononi.
Kwa mujibu wa Umoja wa Afrika, karibu theluthi moja ya watu wazima barani Afrika wana akaunti za pesa kwa simu.