Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi jana Jumapili hapa Beijing amekutana kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Bw. Ronald Lamola na Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Bibi Yacine Fall.
Katika mazungumzo hayo Bw. Wang Yi amesema China inaunga mkono kithabiti nchi za Afrika kulinda haki yake halali ya kujiendeleza, na iko tayari kushirikiana na Afrika kujenga nchi yenye ncha nyingi ambazo zina usawa na utaratibu, na kutafuta utandawazi wa uchumi dunia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika wa Kusini Bw. Lamola amesema, nchi yake inaunga mkono mipango mfululizo ya kimataifa ya China, na kupenda kushirikiana na China kuhimiza kwa pamoja mshikamano na ushirikiano kati ya nchi za “Dunia ya Kusini”.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Bibi Fall amesema wakati wa mkutano huo atafanya ziara ya kitaifa nchini China, ambayo pia ni ziara yake ya kwanza nje ya Afrika, na anatarajia kutumia fursa hii kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati kati ya Senegal na China.