Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, ambaye yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka 2024.
Akibainisha kuwa Umoja wa Afrika ni bendera inayoongoza umoja na uimarishaji wa Afrika na jukwaa muhimu la ushirikiano wa kimataifa, Rais Xi amesema China inaunga mkono Umoja huo kuchukua nafasi kubwa zaidi katika maendeleo ya urafiki kati ya China na Afrika.
Amesema China iko tayari kutafuta mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali katika ushirikiano wake na Umoja wa Afrika na kuinua jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja hadi kufikia ngazi mpya.
Rais Xi amesisitiza kuwa China inaichukulia Afrika kuwa kipaumbele kikuu katika diplomasia yake, na inapenda kuongeza mawasiliano ya kisiasa, kuimarisha kuaminiana kimkakati na ushirikiano wa kivitendo, kubadilishana uzoefu wa maendeleo na kukuza maendeleo ya pamoja na Afrika.