Marais wa China na Malawi wakutana mjini Beijing na kufanya mazungumzo kuhusu kuinua uhusiano kati ya nchi zao
2024-09-03 15:07:47| cri

Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na Rais Lazarus Chakwera wa Malawi, ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka 2024.

Viongozi hao wawili wametangaza kwa pamoja kuinua uhusiano kati ya nchi zao kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati.

Rais Xi amesema China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na Malawi kwenye hatua hii mpya, na kukuza maendeleo ya pamoja na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.