Awamu ya pili ya Maonyesho ya filamu ya “Afrika kwenye Filamu” yamefunguliwa tarehe 2 Septemba katika chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing. Kwenye shughuli hiyo wamealikwa watengenezaji filamu kutoka Nigeria, Tanzania, Ethiopia, Benin na nchi nyingine za Afrika kuleta filamu zao na kuwaelezea vijana wa China hadithi mbalimbali za Afrika, na kuanzisha ukurasa mpya wa mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika.
Mkurugenzi wa kituo cha kutafsiri na kutengeneza filamu na tamthilia cha Shirika kuu la utangazaji la China CMG Bibi Wang Lu amesema kila mwaka shirika lao linaandaa shughuli mbalimbali za mawasiliano ya filamu na tamthilia kati ya China na nchi za Afrika, na wenzi wao wamekuwa wengi zaidi siku hadi siku, hali ambayo imethibitisha msemo wa Afrika kwamba “mtu mmoja anaweza kutembea kwa haraka, bali watu wengi wanaweza kutembea mbali zaidi.
Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Hamis Musa Omar ametoa pongezi kwa video, na kulishukuru shirika la CMG kwa kuandaa shughuli hiyo.