China yapenda kushirikiana na Afrika kutekeleza mipango 10 ya kuendeleza mambo ya kisasa
2024-09-05 11:17:25| cri

Rais Xi Jinping leo tarehe 5 amehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mjini Beijing.

Xi Jinping ameeleza kuwa China na Afrika zinachukua theluthi moja ya watu wote duniani, na bila ya China na Afrika kuwa ya kisasa, hakutakuwa na dunia ya kisasa. Katika miaka mitatu ijayo, China inapenda kushirikiana na Afrika kutekeleza mipango 10 ya ushirikiano kati ya China na Afrika ya kuendeleza mambo ya kisasa ya kukuza kufunzana kuhusu ustaarabu wa kisasa, ustawi wa biashara, mlolongo wa viwanda, mafungamano ya mawasiliano, maendeleo, afya, kilimo, mawasiliano ya watu, nishati za kijani na usalama ili kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika na kuongoza mambo ya kisasa ya nchi za Kusini.