China na Afrika zatarajia kushirikiana kutimiza mambo ya kisasa katika pande sita
2024-09-05 11:17:58| cri

Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika tarehe 5 asubuhi.

Amesema kuwa, nchi za Afrika zinasukuma mbele lengo lake la kutimiza mambo ya kisasa la Ajenda ya mwaka 2063. Na China na Afrika kutaka kutimiza ndoto zao za mambo ya kisasa kwa pamoja, hakika kutaanzisha wimbi la mambo ya kisasa la nchi za Kusini, na kufungua ukurasa mpya wa kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.  

Ameongeza kuwa, China na Afrika zinapaswa kushirikiana kutimiza mambo ya kisasa katika pande sita, yaani kushirikiana kuhimiza mambo ya kisasa yenye haki na usawa, kushirikiana kuhimiza mambo ya kisasa yenye uwazi na kunufaishana, kushirikiana kuhimiza mambo ya kisasa yanayotoa kipaumbele maslahi ya wananchi, kushirikiana kuhimiza mambo ya kisasa yenye ujumuishi, na kushirikiana kuhimiza mambo ya kisasa yanayosaidia uhifadhi wa mazingira, pamoja na kushirikiana kuhimiza mambo ya kisasa yenye amani na usalama.