Xi afanya mazungumzo na rais wa Jamhuri ya Kongo
2024-09-06 14:38:19| cri

Rais Xi Jinping wa China leo amefanya mazungumzo na mwenzake wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso, ambaye yuko Beijing kuhudhuria mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kwa mwaka wa 2024 na kufanya ziara nchini China.

Xi ameipongeza Jamhuri ya Kongo kuwa mwenyekiti mwenza wa FOCAC.