Mashambulizi ya kikosi cha RSF yasababisha vifo vya watu wasiopungua 20 eneo la kati la Sudan
2024-09-09 09:11:30| CRI

Raia zaidi ya 20 wamefariki na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) Jumapili katika mji wa Sinnar katikati mwa Sudan.

Kundi moja la shughuli za kujitolea limesema kikosi hicho kilishambulia kwa mizinga soko la Sinnar na makazi ya Al-Muwazafeen.

Tangu mwezi Juni mwaka huu, kikosi cha RSF kimedhibiti maeneo makubwa ya jimbo la Sinnar huku jeshi la Sudan likidhibiti eneo la mashariki mwa jimbo hilo. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji limekadiria kuwa mapigano hayo katika eneo la Sinnar yamesababisha watu zaidi ya laki 7.25 kukimbia makazi yao.