Kenya imetoa wito kwa serikali za Afrika Mashariki kuongeza uwekezaji katika mikakati ya usalama wa mtandao internet ili kulinda vyama vya ushirika vya akiba na mikopo (SACCOs) dhidi ya tishio linaloongezeka kwenye mtandao wa internet.
Waziri anayeshughulikia Vyama vya Ushirika na Biashara Ndogo na za Kati (MSMEs) wa Kenya Bw. Wycliffe Oparanya, amesisitiza jukumu muhimu ambalo SACCOs inatekeleza katika utulivu wa kiuchumi kwenye nchi nyingi za Afrika, na kutaka serikali zitoe kipaumbele katika utekelezaji wa mifumo ya usalama wa mtandao wa internet kwa kukuza ushirikiano na wadau wa ndani na wa kimataifa.
Kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bibi Susan Mang'eli, Bw. Oparanya pia amesisitiza haja ya kuongeza uelewa, kujenga uwezo, na maendeleo ya mifumo ya tahadhari ya mapema ili kugundua na kukabiliana na hatari za mtandao wa Internet.