Mkutano wa kitaifa wa elimu wa China umefanyika kuanzia tarehe 9 hadi 10 hapa Beijing, ambapo rais Xi Jinping amehudhuria na kutoa hotuba muhimu.
Tarehe 10 Septemba ni maadhimisho ya miaka 40 ya siku ya walimu nchini China, ambapo rais Xi kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ametoa salamu za pongezi kwa walimu na wafanyakazi wote wa mambo ya elimu kote nchini. Amesisitiza kuwa, ni mila nzuri kwa China kuwaheshimu walimu, na kwamba ni muhimu kuboresha hadhi ya kisiasa, kijamii na kitaaluma ya walimu, kuimarisha utoaji wa mishahara kwa walimu, kuongeza kiwango cha ruzuku kwa walimu wa shule za msingi na sekondari, kutekeleza vizuri sera ya utoaji wa posho ya maisha kwa walimu wa vijijini, na kukuza mageuzi ya mishahara ya walimu wa vyuo vikuu. Kulinda heshima ya kazi na maslahi na haki halali ya walimu, kupunguza mizigo ya kazi ya walimu zisizohusiana na elimu na ufundishaji, na kushughulikia vizuri kazi ya kustaafu kwa walimu. Aidha kazi ya utoaji pongezi na utangazaji kwa walimu bora inatakiwa kuimarishwa, ili kuwawezesha walimu wapate heshima kubwa katika jamii na kuifanya kazi ya ualimu kuwa moja kati ya ajira zinazoheshimiwa zaidi.