Balozi wa China nchini Zambia Han Jing amesema, China iko tayari kuisaidia Zambia kufungua mustakbali wake wa maendeleo.
Akiongea kwenye mkutano na wanahabari jana Jumatano mjini Lusaka kuhusu matokeo ya Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mjini Beijing, Balozi Han Jing amesema China iko tayari kutoa uzoefu na fursa za maendeleo yake kwa Zambia, ili kufungua mustakbali mkubwa wa nchi hiyo wa mageuzi ya kiuchumi na kijamii yatakayoongeza tija ya uzalishaji, nyongeza kubwa ya thamani, ustahimilivu na ushirikishi wa kidijitali.
Balozi Han amesema China inahamasisha kampuni za China kushirikiana na washirika wa Zambia katika nishati ya jua na usimamizi wa maji, ili kuisaidia nchi hiyo kutatua msukosuko wa umeme.