China yatoa msaada wa tani 1,300 za chakula kwa Somalia
2024-09-13 09:25:19| CRI

Ubalozi wa China nchini Somalia umetoa msaada wa tani 1,300 za chakula kwa Shirika la Usimamizi wa Majanga la Somalia (SoDMA) ambalo linafanya juhudi kupunguza athari za janga la ukame unaokadiriwa kuendelea kwa muda mrefu.

Balozi wa China nchini humo Wang Yu alipohudhuria hafla ya kukabidhi msaada huo, ameeleza ahadi ya serikali ya China ya kuwaunga mkono watu wa Somalia katika nyakati za changamoto, haswa wakati ukame wa La Nina.

Kamishna wa SoDMA Mahamud Moallim ametoa shukrani kwa watu na serikali ya China akisema msaada huo utatoa ahueni kwa mamilioni ya Wasomali wanaokabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula kutokana na mzunguko usiokoma wa ukame na mafuriko.