Wizara ya Usalama na Ulinzi wa Raia ya Mali ilisema Jumanne kwamba majaribio ya magaidi kushambulia kambi za shule za kijeshi huko Faladie mjini Bamako, nchini Mali, yamezimwa na hali imedhibitiwa.
Wizara hiyo iliwahakikishia wakazi kwamba "hali imedhibitiwa kikamilifu" na kuwataka waendelee na shughuli zao kwa uhuru.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, mashambulizi ya risasi yalifanyika kwenye kambi ya wanajeshi karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Modibo Keita, kilomita 15 kusini mwa mji wa Bamako kwenye mishale ya saa 11 alfajiri kwa saa za huko. Vyanzo vya ndani vinasema hadi sasa barabara katika eneo hilo zimefungwa
Tangu mwaka 2012, Mali imekuwa ikikabiliwa na mzozo mbalimbali kwa njia ya uasi wa kudai uhuru na wapiganaji wa wanajihadi, pamoja na ghasia kati ya jamii, ambazo zimesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na mamia ya maelfu wengine kuhama makazi yao.