China yatoa wito wa kuinua ushirikiano wa pande zote katika kiwango kipya na Ethiopia
2024-09-25 08:38:41| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ametoa wito kwa China na Ethiopia kuinua ushirikiano wa nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali hadi kufikia katika kiwango kipya.

Wang ametoa kauli hiyo katika mazungumzo kati kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Taye Atske Selassie. Katika mazungumzo hayo, Wang amezitaka pande hizo mbili kufuata makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili na kutumia fursa ya kutekeleza matokeo ya Mkutano wa mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ili kuinua ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika nyanja mbalimbali hadi kufikia ngazi mpya.

Kwa upande wake, Taye amesema Ethiopia inathamini uhusiano kati yake na China, na kufuatilia kwa dhati sera ya kuwepo kwa China moja, na kuongeza kuwa nchi yake inatarajia kupanua ushirikiano katika nyanja mbalimbali na kupata matokeo mapya.

Akizungumzia masuala ya kimataifa na kikanda, Taye amesema Ethiopia iko tayari kuimarisha uratibu na ushirikiano na China, kupambana kwa pamoja utaratibu wa upande mmoja na Umwamba, ili kulinda haki na usawa wa kimataifa.