Kiongozi mkuu wa Iran asema Marekani ni “mpangaji mkuu” wa mapambano kati ya Israel na Palestina na kati ya Israel na Lebanon
2024-09-26 23:01:53| cri

Kiongozi mkuu wa Iran Seyyed Ali Khamenei tarehe 25 Septemba alitoa hotuba akisema, mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Lebanon yaliyofanywa hivi karibuni na jeshi la Israel hayatarudisha nyuma kundi la Hezbollah la Lebanon, Israel haitafaulu kwenye vita hiyo. Pia ameishutumu Marekani kuwa ni “mpangaji mkuu” wa mapambano kati ya Israel na Palestina na hali mbaya zaidi kati ya Israel na Lebanon.

Khamenei amesema ingawa kundi la Hezbollah la Lebanon limepoteza baadhi ya makamanda waandamizi hivi karibuni kwenye mashambulizi ya Israel, lakini kundi hilo bado lina uwezo na watu kwa vita, na halitarudi nyuma.

Mbali na hayo, Khamenei amepinga kauli ya Marekani kuwa “Marekani haikushiriki kwenye mpango wa Israel katika kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya Lebanon”.