Xi Jinping atuma salamu za pongezi kwa Ishiba Shigeru kwa kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Japan
2024-10-02 14:23:58| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana alimpigia simu Ishiba Shigeru na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Japan.

Rais Xi amesema kuwa China na Japan ni majirani waliotenganishwa na maji. Nchi hizo mbili zinafuata njia ya kuishi pamoja kwa amani, urafiki wa kudumu, ushirikiano wa kunufaishana na maendeleo ya pamoja, zinazolingana na maslahi ya kimsingi ya watu wa nchi hizo mbili. Inatarajiwa kuwa Japan na China zitaendana pamoja, kuzingatia kanuni na maafikiano ya hati nne za kisiasa kati ya China na Japan, kuhimiza kwa kina uhusiano wa kimkakati na wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili, na kuwa na azma ya kujenga uhusiano thabiti wa China na Japan unaokidhi matakwa ya zama mpya.

Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu Li Qiang pia alituma salamu za pongezi kwa Ishiba Shigeru, akisema kwamba pande hizo mbili zinapaswa kudumisha msingi wa kisiasa wa uhusiano wa nchi hizo mbili, kuimarisha urafiki, kuaminiana na kushirikiana, na kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.