Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres tarehe 13 Oktoba alitoa taarifa kuhusu kikosi cha muda cha UM nchini Lebanon, akiweka bayana msimamo kuwa watu na kambi ya kikosi cha muda cha UM nchini Lebanon hawapaswi kuwa shabaha ya mashambulizi, mashambulizi dhidi ya walinzi wa amani yanakiuka sheria ya kimataifa na sheria ya kibinadamu ya kimataifa, kitendo ambacho huenda kitakuwa uhalifu wa vita.
Bw. Guterres amesisitiza tena kuwa ni lazima kuhakikisha usalama wa wafanyakazi na mali za Umoja wa Mataifa, na ni lazima kuheshimu wakati wote bila masharti kanuni ya kutoshambuliwa kwa kambi za UM.