Ripoti ya pamoja iliyotolewa na Kituo cha Kitaifa cha Kukabiliana na Dharura ya Virusi vya Kompyuta cha China, Maabara ya Kitaifa ya Uhandisi ya Teknolojia ya Kuzuia Virusi vya Kompyuta, na Kampuni ya 360 imesema Marekani ilimetoa taarifa zisizo sahihi kwa shirika la "Volt Typhoon" na kuficha mashambulizi yake ya mtandao kwa kupata matope nchi nyingine.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Bibi Mao Ning jana amesema, mashirika husika ya China yametoa ripoti mbili hapo awali zilizofichua kwamba "Volt Typhoon" ni programu ya kompyuta ya utapeli ambayo inatumiwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na kampuni za usalama za mtandao kueneza habari zisizo za kweli kuhusu China ili kupata fungu la bajeti ya serikali. .
Bibi Mao amesema China inalaani kitendo hicho cha Marekani cha kutowajibika ipasavyo na kuitaka nchi hiyo kuacha mara moja kufanya mashambulizi ya mtandaoni duniani na kuacha kutumia masuala ya usalama wa mtandao kuichafua China.