Uchunguzi wa COMESA Dhidi ya Coca-Cola
2024-10-16 14:41:58| cri

Tume ya Ushindani ya COMESA imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya vitendo visivyo vya ushindani dhidi ya kampuni ya Coca-Cola barani Afrika. Tume hiyo inashuku kuwa Coca-Cola imefanya makubaliano ya usambazaji ambayo yanaweza kuathiri biashara baina ya nchi wanachama. Uchunguzi huo utadumu hadi Novemba 14, 2024, ambapo wadau wametakiwa kuwasilisha maoni yao kwa maandishi.