Wanafunzi wa Rwanda waibuka washindi kwenye mashindano ya Jukwaa la Ulinzi wa Mtandaoni la Afrika
2024-10-18 10:54:06| cri

Vijana wa Rwanda wameibuka washindi katika uzinduzi wa kitaifa wa mashindano ambayo yameundwa kuhamasisha na kuinua ujuzi wa usalama wa mtandao miongoni mwa vijana, wakati huo huo kuongeza juhudi za nchi katika kukuza hadhi yake kama kitovu cha teknolojia kinachojitokeza.

Mashindano hayo ya usalama na ulinzi wa mtandao wa Internet, yalifanyika pembezoni mwa Jukwaa la Ulinzi wa Mtandao wa Internet la Afrika (ACDF). Mashindano hayo yalishirikisha timu kutoka Rwanda kwenye mazingira ya saa 24 ya hali halisi na maabara zinashughulikia changamoto kadhaa, ikiwa ni pamoja na kushambulia mtandao wa internet, uchunguzi wa kidigitali, na ulinzi wa mtandao wa internet.

Timu tatu ziliibuka washindi katika hatua ya kwanza ya mashindano, na viongozi wa mtandao wa internet kutoka barani Afrika walikuwepo kwenye sherehe ya kutoa tuzo.