Waziri wa Madini wa Tanzania Anthony Mavunde amesema kuwa Tanzania inapanga kurudisha minada ya mawe ya thamani ili kuwawezesha wazalishaji na wauzaji wenyeji wa vito vya thamani.
Akizungumza kwenye kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliyokutana mjini Dodoma, Mavunde amesema kuwa minada hiyo itafanyika kila baada ya miezi mitatu katika baadhi ya miji ya Tanzania ikiwemo Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar.
Minada hii itasimamiwa na Tume ya Madini kwa kushirikiana na Tanzania Mercantile Exchange, kwa kutumia mfumo wa mauzo wa kielektroniki. Mawe ya thamani yatakayopatikana kwenye minada ya ndani baadaye yatauzwa katika masoko ya kimataifa.