Uchumi wa kidijitali wa Kenya kuendelea kukua kutokana na motisha wa kiusimamizi: ripoti
2024-10-23 09:27:48| CRI

Uchumi wa kidijitali wa Kenya utakuwa na ukuaji wa kasi katika siku za usoni, ukichochewa na motisha wa kisera na kiusimamizi, ubunifu wa vijana, na kuongezeka kwa mtiririko wa fedha.

Ripoti iliyotolewa jana mjini Nairobi na jumuiya ya GSMA (Global System for Mobile Communications Association)  na washirika wake, inaonyesha kuwa uchumi wa kidijitali utachangia karibu dola bilioni 5.13 za Marekani kwenye pato la taifa la Kenya ifikapo mwaka 2028.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, katibu wa wizara ya habari, mawasiliano na uchumi wa kidijitali Bibi Margaret Ndung'u, amesema kuendeleza mambo ya kidijitali ni ufunguo wa ukuaji endelevu, uundaji wa nafasi za ajira, utoaji wa huduma bora, na ongezeko la mapato ya Kenya.