Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesisitiza maana ya kutumia jukwaa la BRICS kuhimiza maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kati ya nchi wanachama kwenye mkutano wa 16 wa BRICS uliofungwa.
Rais Ramaphosa amesema mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi chini ya mfumo wa BRICS ni majukwaa muhimu kuendeleza uhusiano imara kati ya nchi zilizo Kusini mwa Dunia na masoko yanayoibuka.
Amepongeza mapendekezo ya Russia kuimarisha nchi za BRICS kupitia mipango mbalimbali inayolenga kuboresha siku za baadaye za mitandao ya uchukuzi ya nchi za BRICS na muunganiko chini ya kaulimbiu ya “Ubunifu na Udijitali kwenye Uchukuzi”.
Pia amesisitiza haja ya juhudi za ushirikiano kuhakikisha maslahi ya watu ndani ya kundi la BRICS.