Watu wanne wafariki na wanane kujeruhiwa kwenye ajali ya kugongana kwa ndege ya kuua wadudu na tuk-tuk nchini Sudan
2024-10-28 09:33:52| CRI

Wafanyakazi wanne wa kilimo wamefariki na wengine wanane kujeruhiwa baada ya ndege ya kunyunyizia dawa ya kuua wadudu kugongana na tuk-tuk katika Jimbo la Gedaref mashariki mwa Sudan.

Kaimu Waziri wa Kilimo wa Jimbo la Gedaref Ammar Suleiman amesema ajali hiyo imetokea wakati ndege hiyo ikitua katika eneo la kilimo, huku rubani wake akishangazwa baada ya tuk-tuk kuingia ghafla kwenye barabara ya kurukia ndege.

Wafanyakazi watatu wa ndege hiyo walinusurika katika tukio hilo, huku ndege hiyo ikiharibika kwenye bawa na propela, Suleiman ameongeza kuwa majeruhi wote ni wa tuk-tuk iliyowabeba watu 15 wakati wa ajali hiyo. Jimbo la Gedaref kwa sasa linajiandaa kuanza kwa mavuno ya mazao ya majira ya kiangazi, hasa ufuta.