Roboti zinazoshughulikia kilimo zaongeza ufanisi wa uzalishaji wa kilimo
2021-01-22 16:50:50| cri

Katika uwanja wa majaribio ya kilimo huko Wuzhen, mkoani Zhejiang, roboti zaidi ya aina 40 zinashughulikia mambo mbalimbali ya kilimo, yakiwemo uchukuzi wa matunda, usimamizi wa data mbalimbali, hali ya ukuaji wa mimea, na kazi mbalimbali.

Kutokana na kazi za roboti hizo, ufanisi wa uzalishaji wa kilimo umeboreshwa kwa kiasi kikubwa. Kwa kutumia teknolojia ya Internet of Things, chombo cha utambuzi kinachowekwa chini ya ardhi kinaweza kufuatilia hali ya unyevu wa udongo, na kuwakumbusha wakulima ni wakati wa kumwagilia; data mbalimbali kama joto, unyevu na mwanga pia zinahifadhiwa kupitia mtandao wa Internet, ili kutoa data kwa ajili ya kuhakikisha viwango vya uzalishaji wa kilimo.

Mzunguko wa bidhaa za mazao ya kilimo uliathiriwa vibaya kutokana na janga la virusi vya Corona mwaka 2020, mkuu wa uwanja huo wa majaribio ya kilimo Fu Qian ameeleza kuwa, kupitia teknolojia ya mtandao wa Internet, uwanja huo wa kilimo ulikamilisha mara mbili kazi ya kusafirisha mboga kati ya mkoa wa Shandong na mji wa Shanghai, pamoja na mkoa wa Zhejiang ndani ya saa 48.