Wakati unapopigia simu ya nyumbani kwa rafiki yako wa China, huwa unaweza kusikia kwamba rafiki yako anataka wewe ukipata nafasi uende nyumbani kwake kuongea, maneno hayo huonesha urafiki wake kwako, lakini siyo mwaliko rasmi.
Kutemebeleana kati ya jamaa na marafiki au watu wanaofanya kazi pamoja ni jambo la kawaida nchini China, na kuwaalika wengine haina haja ya kuthibitisha tarehe au saa, kama ukitaka kwenda kumtembelea mmoja, unaweza kumwambia, kama una nafasi unaweza kwenda. Na hivi sasa marafiki au jamaa wamepunguza nafasi za kutembeleana, na watu wengi wanapenda kuwasiliana au kusalimiana kwa kutumia ujumbe kwenye simu za mikononi na kuandika e-mail.