somo 47 Kutibiwa na madaktari

 ongea na CRI
 

Matibabu ya kichina ni njia maalum na mfumo maalum wa matibabu nchini China, matibabu ya kichina yana maana ya kina ya kifalsafa, matibabu ya kichina yanatilia maanani kuthibisha dalili za magonjwa kutoka hali ya jumla ya mwili mwa mtu, halafu kuzingatia njia mbalimbali zinazosaidia katika matibabu. Elimu ya matibabu ya kichina inaona kuwa, mwilini mwa binadamu kuna mishipa ya viungo, kwa mtu mwenye afya nzuri, hali ya uwiano kati ya mwili na viungo vya mwili inadumishwa, kama hakuna uwiano kati ya mwili na viungo vya mwili, dalili za ugonjwa zitaonekana, na mtu atapatwa na ugonjwa. Daktari wa matibabu ya kichina anapokutana na mgonjwa kwanza anaangalia sura yake, hali ya mwilini wake, kuchunguza hali ya mishipa ya viungo, halafu kuzingatia hali ya afya ya mgonjwa, desturi zake za chakula, majira ya kupatwa na ugonjwa, hali ya hewa ya sehemu tofauti na sababu nyingine. Hata kwa watu waliopata ugonjwa wa namna moja, daktari huweza kuwaandikia dawa tofauti.