Nchini China, maktaba zinatapakaa kwenye sehemu mbalimbali, na maktaba kubwa zaidi ni Maktaba ya taifa ya China iliyoko mjini Beijing. Hiyo ni maktaba inayohifadhi vitabu na nyaraka za lugha ya Kichina nyingi zaidi kuliko zile za maktaba nyingine duniani, pia ni maktaba inayohifadhi vitabu na majarida ya lugha za kigeni mengi zaidi kuliko maktaba nyingine nchini China. Katika maktaba hiyo ya taifa ya China, yanahifadhiwa maandishi yaliyochongwa kwenye magamba ya kobe yaliyofukuliwa kutoka sehemu ya Yinxu ambayo ni mabaki ya mji wa kale wa kipindi cha mwisho cha Enzi ya Shang ya zaidi ya miaka 3000 iliyopita. Hivi sasa maktaba hiyo kila siku inafunguliwa kwa wasomaji, kwa wastani, kila siku inapokea wasomaji elfu 13.6.