Ili kuanzisha harakati za umma za kujenga mwili, vifaa na zana vya michezo vimefungwa kwenye maeneo mengi ya wakazi au katika mabustani, wakazi wakitoka nyumbani watafanya mazoezi ya kujenga mwili kwenye sehemu zilizo karibu na nyumbani kwao. Wachina wametambua zaidi umuhimu wa kujenga mwili, na kuna njia nyingi za kushiriki kwenye michezo, watu wanaweza kuchagua njia zinazowafaa kutokana na kiwango chao cha mapato na michezo wanayopenda.