Mgawanyo wa mikoa ya utawala
Utaratibu wa sehemu za utawala
Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China inasema kuwa, sehemu za utawala za China zinagawika kama zifuatazo:
( 1 ) Nchi nzima imegawanywa katika mikoa, mikoa inayojiendesha na miji inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu.
( 2 ) Mikoa na mikoa inayojiendesha inagawanyika kuwa majimbo, wilaya, wilaya zinazojiendesha na miji.
( 3 ) Wilaya, wilaya zinazojiendesha na miji inagawanyika kuwa tarafa, tarafa za kikabila na miji ya wilaya.
Mikoa inayojiendesha, majimbo yanayojiendesha na wilaya zinazojiendesha zote ni sehemu zinazojiendesha za makabila madogomadogo.
Serikali kuu inaweza kuanzisha mkoa wa utawala maalum wakati kuna haja ya lazima.
Hivi sasa China ina sehemu 34 za utawala wa ngazi ya mikoa, pamoja na miji minne inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu, mikoa 23, majimbo matano yanayojiendesha, na mikoa miwili ya utawala maalum.
Sehemu za utawala wa ngazi za mikoa za China
Beijing
Beijing ni mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, ambao unaitwa pia kuwa Jing kwa ufupi. Beijing iko kwenye ncha ya kaskazini magharibi ya Tambarare ya Huabei. Mwanzoni Beijing iliitwa kuwa Ji, na ilikuwa mji mkuu wa Dola la Yan wakati wa madola ya vita ya Chunqiu, na iliwahi kuwa mji mkuu wa pili wa Enzi ya Liao na kuitwa kuwa Yanjing. Beijing ilikuwa mji mkuu katika Enzi za Jin, Yuan, Ming na Qing na mwanzoni mwa Mingguo. Iliwahi kuitwa kuwa Zhongdu, Dadu, Beiping na Beijing. Beijing iliwekwa kuwa mji kuanzia mwaka 1928. Hivi sasa mji huo una manispaa 16 na wilaya mbili, na ni mji unaotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu. Eneo la mji mzima ni kilomita za mraba 1.68. Mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya watu wenye kadi za ukazi ilikuwa milioni 11.363. Beijing ni kituo cha kisiasa cha China pia ni kituo cha utamaduni, sayansi na elimu na sehemu muhimu ya mawasiliano. Aidha, Beijing ni sehemu yenye vivutio vingi vya utalii vinavyojulikana nchini na ng'ambo, vivutio hivyo ni pamoja na Ukuta mkuu, masri ya wafalme wa kale, Bustani ya Tiantan, Makaburi ya wafalme 13, hekalu la majira ya joto na Mlima Xiangshan.
Shanghai
Shanghai inaitwa Hu kwa ufupi. Shanghai iko kwenye sehemu ya katikati ya pwani ya mashariki ya China na sehemu ya mlango wa kuingia baharini kwa maji ya Mto Changjiang. Katika zama za kale, sehemu hiyo ilikuwa kijiji cha wavuvi cha kando ya bahari, ambayo ilikuwa sehemu ya Dola ya Wu wakati wa Enzi ya madola ya vita ya Chunqiu, na ilikuwa mji wa wilaya wakati wa Enzi ya Son, ilianza kuitwa Shanghai, na kuibuka kuwa mji kuanzia mwaka 1927. Hivi sasa Shanghai ni mmoja kati ya miji mikubwa minne inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu ya China, mji huo una minispaa 18 na wilaya moja. Eneo la mji mzima ni kilomita za mraba 5800. Hadi mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya watu wa mji huo ilikuwa milioni 13.347. Shanghai ni mji mkubwa wa kwanza wa China, pia ni mmoja kati ya miji mikubwa duniani. Shanghai pia ni mji wa viwanda ulio mkubwa zaidi kuliko mingine ya China, pia ni kituo cha biashara, fedha na sayansi na teknolojia.
Tianjin
Tianjin inaitwa Jin kwa ufupi. Tianjin iko kwenye sehemu ya kaskazini mashariki ya Tambarare ya Huabei, na kwenye sehemu ya makutano ya matawi matano ya Mto Huai. Iliitwa Zhigu katika Enzi ya Jin, ambayo ilikuwa sehemu muhimu ya usafiri wa meli, baadaye iliwekwa kuwa mji wa wilaya ya Haijin, na mwanzoni mwa Enzi ya Ming iliitwa kuwa Tianjin, na ilikuwa mji wa Tianjin kuanzia mwaka 1928. Hivi sasa Tinjian ina minispa 15 na wilaya 3, Tinjian ni mji unaotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu. Eneo la mji mzima ni kilomita za mraba zaidi ya elfu 11. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya watu wa mji huo ilikuwa milioni 9.1905. Tianjin ni mji mkubwa kabisa wa viwanda kwenye sehemu ya kaskazini ya China, mji huo una maliasili nyingi ya mafuta na gesi, na chumvi zilizotengenezwa kwa maji ya baharini, mji huo pia una msingi imara kiasi wa teknolojia za viwanda, vilevile ni kituo muhimu cha biashara na bandari katika sehemu ya kaskazini ya China. Mji huo una vivutio vya utalii kama vile Bustani ya Ning, Jumba la malkia, Kituo cha mizinga cha Dagu, Hekalu la Dule la wilaya ya Ji, Ukuta mkuu wa kale wa mlango wa Huangya na sehemu ya Mlima Pang yenye mandhari nzuri.
Chongqing
Chongqing unaitwa Yu kwa ufupi. Uko mashariki ya sehemu ya kusini magharibi ya China, na kwenye eneo la juu la Mto Changjiang, ilikuwa sehemu ya Dola la Ba wakati wa Madola ya vita ya Chunqiu. Chongqing ilikuwa mji mkuu wa pili wa serikali ya Chama cha Guomindang wakati wa kupambana na uvamizi wa Japan. Mwaka 1997 Chongqing iliamuliwa kuwa mji unaotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu, mji huo una minispa 15, miji midogo minne ya ngazi ya wilaya, pamoja na wilaya 17 na wilaya 4 inayojiendesha ya makabila madogomadogo. Eneo la mji mzima ni kilomita za mraba elfu 82.3. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya jumla ya watu wa mji huo ilikuwa milioni 31.07. Chongqing ni mji wa viwada vya mseto, sehemu hiyo ina vivutio vya utalii kama vile Magenge matatu ya Mto Changjian, Mlima Pipa na Mlima Jinyun.
Hebei
Mkoa wa Hebei unaitwa Ji kwa ufupi, uko kwenye sehemu ya kaskazini ya China, mkoa huo unakaribia na Bahari Bo. Eneo la mkoa huo ni kilomita za mraba laki 1.9. Idadi ya watu ni milioni 67.346. Mji mkuu wa mkoa huo ni Shijiazhuan.
Shanxi
Mkoa wa Shanxi unaitwa Jin kwa ufupi, uko kwenye sehemu ya kaskazini ya China na magharibi ya Milima Taihang. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.5. Idadi ya watu ni milioni 32.9371. Mji mkuu wa mkoa huo ni Taiyuan.
Mongolia ya ndani
Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani unaitwa Mongolia ya ndani kwa ufupi, uko kwenye sehemu ya mipaka ya kaskazini ya China, upande wake wa kaskazini unapakana na nchi za Mongolia na Russia. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya milioni 1.1. Idadi ya watu wake ni milioni 23.7859. Mji mkuu wa mkoa huo ni Hulhait.
Liaoning
Mkoa wa Liaoning unaitwa Liao kwa ufupi, uko kusini mwa sehemu ya kaskazini ya mashariki ya China, upande wake wa kusini unakaribia Bahari Bo na Bahari Huang, upande wake wa mashariki unapakana na Korea ya kaskazini. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.5. Idadi ya watu wake ni milioni 42.03. Mji mkuu wa mkoa huo ni Shenyang.
Jilin
Mkoa wa Jilin unaitwa kuwa Ji kwa ufupi, uko katikati ya sehemu ya kaskazini mashariki ya China, upande wake wa kusini mashariki unapakana na Russia na Korea ya kaskazini. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.8. Idadi ya watu wa mkoa huo ni milioni 26.994. Mji mkuu wa mkoa huo ni Changchun.
Heilongjiang
Mkoa wa Heilongjiang unaitwa Hei kwa ufupi, uko kaskazini kabisa ya sehemu ya kaskazini mashariki ya China, upande wake wa mashariki na wa kaskazini zinapakana na Russia. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 4.6. Idara ya watu wake ni milioni 38.13. Mji mkuu wa mkoa huo ni Harbin.
Jiangsu
Mkoa wa Jiangsu unaitwa Su kwa ufupi, uko kwenye eneo la chini la Moto Changjiang na Mto Hui, na kando ya Bahari Huang. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki moja. Idadi ya watu wa mkoa huo ni milioni 71.273. Mji mkuu wa mkoa huo ni Nanjing.
Zhejiang
Mkoa wa Zhejiang unaitwa Zhe kwa ufupi, uko katikati ya sehemu ya mashariki ya China na kando ya Bahari ya Dong. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki moja. Idadi ya watu wake ni milioni 46.47. Mji mkuu wa mkoa huo ni Hangzhou.
Anhui
Mkoa wa Anhui unaitwa Wan kwa ufupi, ambao uko kaskazini magharibi ya sehemu ya mashariki ya China, mkoa huo unapita Mto Changjiang na Mto Huai. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.3. Idadi ya watu wake ni milioni 63.68. Mji mkuu wa mkoa huo ni Hefei.
Fujian
Mkoa wa Fujian unaitwa Min kwa ufupi, uko kwenye pwani ya kusini mashariki ya China, mkoa huo unakabiliana na mkoa wa Taiwan kwa bahari. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.2. Idadi ya watu wake ni milioni 34.66. Mji mkuu wa mkoa huo ni Fuzhou.
Jiangxi
Mkoa wa Jiangxi unaitwa Gan kwa ufupi, uko kwenye kando ya kusini ya eneo la katikati na la chini la Mto Changjiang. Eneo la mkoa huo ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.6. Idadi ya watu wake ni milioni 42.2243. Mji mkuu wa mkoa huo ni Nanchang.
Shandong
Mkoa wa Shandong unaitwa Lu,o uko kwenye eneo la chini la Mto Huang, unakaribia Bahari Huang na Bahari Bo. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.5. Idadi ya watu wake ni milioni 90.82. Mji mkuu wa mkoa huo ni Jinan.
Henan
Mkoa wa Henan kwa ufupi unaitwa Yu, uko kwenye eneo la katikati na la chini ya Mto Huang, ulikuwa sehemu ya "Zhongyuan" katika zama za kale. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.6. Idadi ya watu wake ni milioni 96.13. Mji mkuu wa mkoa huo ni Zhengzhou.
Hubei
Mkoa wa Hubei unaitwa E, ambao uko katika eneo la katikati la Mto Changjiang, na kaskazini ya Ziwa Dongting. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.8. Idadi ya watu wake ni milioni 59.878. Mji mkuu wa mkoa huo ni Wuhan.
Hunan
Mkoa wa Hunan unaitwa Xiang, ambao uko kwenye kando ya kusini ya eneo la katikati ya Mto Changjiang, sehemu kubwa ya mkoa huo iko kusini ya Ziwa Dongting. Eneo la mkoa huo ni kilomita za mraba zaidi ya laki 2.1. Idadi ya watu wake ni milioni 66.285. Mji mkuu wa mkoa huo ni Changsha.
Guangdong
Mkoa wa Guangdong unaitwa Yue, ambao uko kusini mwa Mlima Nanling, na kwenye kando ya Bahari ya kusini. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.8. Idadi ya watu wake ni milioni 78.5858. Mji mkuu wa mkoa huo ni Guangzhou.
Guangxi
Mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuan wa Guangxi unaitwa Gui kwa ufupi, uko magharibi ya sehemu ya kusini ya China, upande wake wa kusini unakaribia Ghuba ya Beibu, sehemu ya kusini magharibi ya mkoa huo inapakana na Vietnam. Eneo la mkoa huo ni kilomita za mraba zaidi ya laki 2.3. Idadi ya watu wake ni milioni 48.22. Mji mkuu ni Nanning.
Hainan
Mkoa wa Hainan unaitwa Qiong, ambao uko pwani ya kusini mwa China, upande wake wa kaskazini unakabiliana na Mkoa wa Guangdong, kati yao ni Mlango wa bahari wa Qiongzhou. Mkoa huo una Kisiwa cha Hainan, Visiwa vya Xisha, Visiwa vya Nansha, Visiwa vya Zhongsha na eneo lake la mamlaka ya bahari. Eneo la nchi kavu la mkoa huo ni kilomita za mraba zaidi ya elfu 34. Idadi ya watu wake ni milioni 8.0313. Mji mkuu wa mkoa huo ni Haikou.
Sichuan
Mkoa wa Sichuan unaitwa Chuan au Shu, ambao uko kwenye sehemu ya kusini magharibi ya China na eneo la juu la Mto Changjiang. Eneo lake ni kilomita za mraba laki 4.8. Idadi ya watu wake ni milioni 86.733. Mji wake mkuu ni Chengdu.
Guizhou
Mkoa wa Guizhou kwa ufupi unaitwa Qian au Gui, uko mashariki ya Uwanda wa juu wa Yunnan na Guizhou wa kusini magharibi ya China. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.7. Idadi ya watu wake ni milioni 38.3728. Mji mkuu wa mkoa huo ni Guiyang.
Tibet
Mkoa unaojiendesha wa Tibet unaoitwa Zang, uko kwenye Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, na unapakana na India, Nipel, Buthan, na Myanmar. Eneo lake ni zaidi ya kilomita za mraba 120, idadi ya watu wake ni milioni 2.63. Mji mkuu wake ni Lahsa.
Yunnan
Mkoa wa Yunnan unaitwa Dian au Yun, uko kwenye sehemu ya mpaka wa kusini magharibi ya China, na unapakana na Myanmar, Laos na Vienam. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 3.8. Idadi ya watu wake ni milioni 43.331. Mji mkuu wake ni Kunming.
Shanxi
Mkoa wa Shanxi unaitwa Shan au Qin,uko kwenye eneo la katikati ya Mto Huanghe. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 1.9. Idadi ya watu wake ni milioni 36.737. Mji mkuu ni Xian.
Gansu
Mkoa wa Gansu unaitwa Gan au Long, ambao uko kwenye eneo la katikati la Mto Huang, kaskaizni magharibi ya China, sehemu moja ya upande wake wa kaskazini magharibi inapakana na Mongolia. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 3.9. Idadi ya watu wake ni milioni 25.9258. Mji mkuu ni Lanzhou.
Qinghai
Mkoa wa Qinghai unaitwa Qing, ambao uko kaskazini magharibi ya China na kwenye eneo la juu la Mto Changjiang na Mto Huanghe. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya laki 7.2. Idadi ya watu wake ni milioni 5.286. Mji mkuu wa mkoa huo ni Xining.
Ningxia
Mkoa unaojiendesha wa kabila la wahui wa Ningxia unaitwa Ning, ambao uko kwenye eneo la katikati la Mto Huanghe, kaskazini magharibi ya China. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi la elfu 66. Idadi ya watu wake ni milioni 5.7154. Mji mkuu wa mkoa huo ni Yinchuan.
Xinjiang
Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyrgu unaitwa Xin, ambao uko kwenye sehemu ya mipaka ya kaskazini magharibi ya China, mkoa huo unapakana na Mongolia, Russia, Kazakstan, Kyrgyzstan, Tajikstan, Afghanistan, Pakistan na India. Eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya milioni 1.6, ni mkoa wenye eneo kubwa zaidi kuliko mingine nchini China. Idadi ya watu wake ni milioni 19.0519. Mji mkuu wa mkoa huo ni Urmuqi.
Taiwan
Mkoa wa Taiwan unaitwa Tai, ambao uko kwenye sehemu ya rafu inayoelekea pwani ya kusini mashariki ya China, Taiwan ni kisiwa kikubwa cha kwanza cha China, upande wake wa mashariki unakaribia Bahari ya Pasifiki, kaskazini mashariki inapakana na Visiwa vya Liuqiu, kusini kupakana na Mlango wa bahari wa Bash. Sehemu yake ya kusini inakabiliana na Mkoa wa Fujian, kati yao ni Mlango wa bahari wa Taiwan. Eneo lake ni kilomita za mraba elfu 36. Idara husika ya Taiwan ilitoa takwimu zikionesha kuwa, hadi mwezi Agosti mwaka 2002, idadi ya watu wa Mkoa wa Taiwan ni zaidi ya milioni 22.4, na idadi ya jumla ya watu wake ni milioni 22.48 wakiwemo watu wa Jinmen na Mazu. Mji mkuu wa Mkoa wa Taiwan ni Taibei.
Hongkong
China ilirudisha mamlaka yake huko Hongkong kuanzia tarehe 1 Julai mwaka 1997, na ikaanzisha Mkoa wa utawala maalum wa Hongkong. Hongkong inaitwa Gang kwa ufupi , ambao uko kwenye pwani ya Bahari ya kusini na upande wa mashariki ya Mlango wa Mto Zhujing, kusini ya mji Shenzhen wa Mkoa wa Guangdong. Hongkong ina kisiwa cha Hongkong, visiwa vya Jiulong na Xinjie pamoja na vingine vilivyoko karibu navyo. Eneo la jumla la Hongkong ni kilomita za mraba 1098.51. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya jumla ya watu wa Hongkong ilikuwa milioni 6.8158, miongoni mwao wakazi wa kudumu ni milioni 6.6253, na wakazi wanaohamahama ni laki 1.905 .
|