9: Hifadhi ya Mazingira

Hatua za hifadhi ya mazingira

Kushughulikia hali ya uchafuzi

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya China imethibitisha sehemu kadha wa kadha zinazotakiwa kushughulikiwa hali ya uchafuzi, kutunga na kutekeleza mipango ya kushughulikia uchafuzi wa maji kwenye eneo la mtiririko wa mito, sera za usimamizi na sera za udhibiti wa jumla wa utoaji wa maji taka. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2002, serikali ya China imetenga fedha za renminbi zaidi ya yuan bilioni 40 katika hifadhi ya mazingira ya sehemu ya Bwawa la Magenge Matatu ya Mto Changjiang na eneo la boma. Mwaka 2001, kwenye eneo la Bwawa la Magenge Matatu ya Mto Changjiang, vyanzo vilivyosababisha uchafuzi vilipungua kwa 37, na viwanda 60 vilivyoko kwenye eneo hilo, utoaji wa maji taka ulipungua kwa 15.6 % kuliko mwaka 2000; ujumla wa utaoji wa takataka za aina mbalimbali ulikuwa tani elfu 8. Kuanzia mwaka 2002, eneo la Ziwa Taihu lenye uchafuzi mbaya limeshughulikiwa kwa kazi maalum, ambapo Mto Changjiang unatoa maji yake safi kwa ziwa hilo linalopita eneo la kilomita za mraba 36,900. Kuanzishwa kwa mradi huo kumeboresha dhahiri mazingira ya maji ya eneo la Ziwa Taihu, na kupunguza kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa vitu vya kemikali ndani ya maji, hali hiyo imeboresha kidhahiri hali ya maji ya bomba ya mji wa Shanghai na miji mingine, na watu milioni 10 hivi wamenufaika nayo.

Wakati huo huo, ufuatiliaji na upimaji wa hewa umefanyika kote nchini China. Mwaka 2002, sifa ya hewa katika miji ya kote nchini iliendelea kuboreka, ambapo miji 117 kati ya miji 339 iliyofuatiliwa na idara ya hifadhi ya mazingira, sifa ya hewa ilikuwa nzuri zaidi ya kigezo cha kitaifa cha ngazi ya pili, na sifa ya hewa katika miji 10 kama vile Haikou, Sanya na Zhaoqing ilifika kigezo cha ngazi ya kwanza. Kazi ya kushughulikia hewa ya Beijing imepata ufanisi dhahiri, siku zenye hewa nzuri ambayo sifa yake ilifika kigezo cha ngazi ya pili zilikuwa 201 mwaka 2002, hili ni ongezeko la siku 19 kuliko zile za mwaka 2001. Utoaji wa hewa chafu wa magari katika miji mingi nchini China ulifikia kigezo cha kwanza cha Ulaya, mji wa Beijing na miji mingine mikubwa imeanza kufuata kigezo cha pili cha Ulaya.

Hifadhi ya maliasili ya misitu

Tokea miaka ya 50 ya karne ya 20, China ilipanda miti mingi na kujenga eneo la misitu kwa nguvu za binadamu. Tokea mwaka 1981 hadi mwaka 2002, miti iliyopandwa na wananchi wa China ilifikia zaidi ya bilioni 39.8. Hivi sasa eneo la miti iliyopandwa nchini China limefikia hekta milioni 46.67, eneo hili ni 26 % ya lile la jumla ya eneo la miti iliyopandwa duniani, linachukua nafasi ya kwanza duniani, na eneo la misitu la China limefikia 16.55 %. Katika hali ambayo maliasili ya misitu duniani inapungua siku hadi siku, China imedumisha upanuzi wa eneo la misitu na idadi ya miti, China imeorodheshwa na Shirika la hifadhi ya mazingira la Umoja wa Mataifa kuwa moja kati ya nchi 15 zenye misitu mingi zaidi duniani.

Tokea mwaka 1998 hadi mwaka 2001, serikali kuu ya China ilitenga yuan bilioni 42.7 katika hifadhi ya misitu na mbuga kwenye sehemu ya magharibi ya kati wanakoishi watu wengi zaidi wenye matatizo ya kiuchumi, kutoa ruzuku kwa wakulima wa huko na kuwahamasisha watu kupanda miti kwenye mashamba yaliyochimbuliwa kupita kiasi, au kupanda majani kwenye mashamba kama hayo ili yawe malisho. Mradi wa kufufua misitu kwenye ardhi za misitu zilizotumiwa kuwa mashamba ya kulima ulianzishwa katika mikoa na miji 25 nchini, ilipofika mwaka 2002, miti imepandwa tena katika ardhi zenye hekta milioni 6.44 zilizotumiwa kuwa mashamba ya kulima. Ufanisi wa hatua ya mwanzo umeonekana, ambapo hali ya mmomonyoko wa ardhi imeboreshwa kwa kiasi fulani. Na kuanzia mwaka 1998, mradi wa kuhifadhi misitu asilia ulianzishwa kote nchini na kupata mafanikio, mradi huo unataka sehemu zote nchini kuacha kukata miti ya misitu ya asili, katika sehemu nyingi, wafanyakazi wa ukataji wa miti wamekuwa walinzi wa misitu.

Kwa kufuata lengo lililowekwa kwenye taarifa ya utafiti wa mikakati ya maendeleo endelevu ya shughuli za misitu za China, ifikapo mwaka 2050, eneo la misitu la China litafika 28 %.

Hifadhi ya ardhi oevu

angu China ijiunge na "Mkataba wa ardhi oevu wa kimataifa" mwaka 1992, serikali ya China imefanya juhudi za kuokoa na kufufua maliasili za ardhi oevu, ardhi oevu asilia kadha wa kadha zilizowahi kuharibiwa zimehifadhiwa. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2002, China imejenga sehemu 353 za hifadhi ya ardhi oevu asilia kote nchini zilizopo kando ya bahari, maziwa na mito na ukingoni mwa misitu, na sehemu 21 miongoni mwao zimeorodheshwa kwenye arodha ya ardhi oevu muhimu duniani, eneo la sehemu hizo limefika hekta milioni 3.03.

"Mpango wa utekelezaji wa hifadhi ya ardhi oevu ya China" unaotekelezwa kuanzia mwezi Novemba mwaka 2000 ulitungwa na wizara 17 za baraza la serikali la China ikiwemo wizara ya misitu ya China. Kutokana na mpango huo, ifikapo mwaka 2010, China itadhibiti mwelekeo wa kudidimia kwa ardhi oevu kutokana na shughuli za binadamu, na ifikapo mwaka 2020, ardhi iliyodidimia au kupotezwa itafufuliwa siku hadi siku.

Kuzuia na kushughulikia ardhi inayobadilika kuwa jangwa

Hali kuhusu ardhi inayobadilika kuwa jangwa imekuwa tatizo moja kati ya matatizo makubwa kabisa ya mazingira ya viumbe nchini China, eneo la ardhi hiyo ya kilomita za mraba 262 kote nchini China limezidi eneo la jumla la mashamba ya kulima nchini kote, hili ni 27 % ya eneo la jumla la ardhi ya China. Hivi sasa ingawa mwelekeo wa ardhi kubadilika kuwa jangwa umedhibitiwa, lakini kila mwaka eneo la ardhi hilo linaongezeka kwa zaidi ya kilomita za mraba 3000.

Idara ya misitu ya taifa imeanza kutekeleza mpango wa kuzuia jangwa na kuondoa hali ya jangwa kote nchini, inajitahidi kudhibiti kimsingi mwelekeo wa kupanuka kwa ardhi ya jangwa ifikapo mwaka 2010; ilipofika mwaka 2003, kwenye msingi wa kuimarisha kazi ya kuondoa jangwa, eneo la jumla la ardhi inayobadilika kuwa jangwa lilianza kupunguza mwaka hadi mwaka; ifikapo mwaka 2050, ardhi zote zenye hali ya jangwa zitashughulikiwa kimsingi ili kujenga mfumo kamili wa viumbe katika ardhi zenye hali ya jangwa.

Hifadhi ya aina nyingi za viumbe

China ikiwa moja kati ya nchi zilizotangulia kusaini "Mkataba wa aina nyingi za viumbe", siku zote inashiriki kwa juhudi katika mambo ya kimataifa yanayohusu mkataba huo, na kutoa maoni kuhusu masuala makubwa ya utekelezaji wa mkataba huo. China vilevile ni moja kati ya nchi chache zilizotangulia kukamilisha mpango wa utekelezaji wa mkataba huo. "Mpango wa China wa utekelezaji wa hifadhi ya aina nyingi za viumbe" uliokamilika mwaka 1994, umezifanya shughuli nyingi za hifadhi ya mazingira ya viumbe ziweze kufanyika kwa kufuata kanuni zilizowekwa kwenye mkataba huo. Kutokana na "Sheria ya hifadhi ya wanyama pori", kitendo chochote cha kuharibu maliasili ya wanyama pori kitaadhibiwa, na mtu atakayefanya uhalifu huo anaweza kuhukumiwa kifo.

Idara husika za serikali zinazingatia sana hifadhi yenye ufanisi ya maliasili za viumbe. Mwezi Januari mwaka 2003, Taasisi ya sayasni ya China ilitetea kuanzisha mradi wa kuokoa mimea inayokabiliwa na hatari ya kutoweka, inapanga kuongeza aina elfu 13 za mimea inayohifadhiwa kwenye bustani 12 za mimea kuwa aina elfu 21, na kujenga bustani kubwa kabisa la mimea duniani lenye eneo la kilomita za mraba 458. Katika mradi huo, fedha za renminbi zaidi ya yuan milioni 300 zitatumika katika kukusanya mimea adimu inayokaribia kutoweka, na kujenga ghala ya gene za mimea katika sehemu muhimu za Milima Qinglin, mji wa Wuhan, Xishuangbanna na Beijing.

Mafanikio ya hatua ya mwanzo yamepatikana katika mradi wa kuokoa wanyama pori wanaokaribia kutoweka, hivi sasa vituo 250 vya kuzaliana kwa wanyama pori vimejengwa nchini kote China, ambapo unatekelezwa mradi maalum wa kuokoa aina 7 za wanyama pori kama vile panda wakubwa na ndege kwarara. Hivi sasa panda wakubwa ambao wamechukuliwa kuwa ni "hazina ya taifa" na kusifiwa kuwa ni "visukuku hai" wamehifadhiwa na kudumishwa kuwa zaidi ya 1000, na mazingira yao ya kuishi yanaendelea kuboreshwa; kundi la ndege ina ya Kwarara mwenye kishungi (crested ibis) limeongezeka kuwa ndege 250 kutoka 7, hali ya kukaribia kutoweka inapungua zaidi; idadi ya mamba wa Yanzi inakaribia elfu 10; (eld's deer) paa wa Hainan imeongezeka na kuwa zaidi ya 700 kutoka 26; kundi la ndege aina ya shakwe wa zamani (relicgull) limeongezeka na kuwa zaidi ya elfu 10 kutoka 2000; chui walioonekana nadra wamejitokeza mara kwa mara katika sehemu ya kaskazini mashariki, mashariki na kusini ya China; kazi ya utafiti kuhusu hali ya kuzaana kwa pomboo wenye mapezi meupe pia inafanyika kwa haraka; Kutokana na kazi isiyolegea ya kupiga vita uwindaji wa haramu, pamoja na kushirikiana na jumuiya kadhaa za kimataifa za hifadhi ya wanyama, swala wa Tibet waliouawa kiharamu na kupungua kwa haraka wamepata nafasi ya kuzaliana katika hali ya utulivu, hivi sasa idadi ya swala wa Tibet imedumishwa kuwa elfu 70 hivi.

Ujenzi wa sehemu ya hifadhi ya maumbile

Hifadhi ya maumbile ya kwanza ya China ilianzishwa kwenye sehemu ya Mlima Dinghu ya Chaoqing mkoani Guangdong mwaka 1956. Hifadhi ya maumbile ya chanzo cha mito mitatu iliyoanzishwa mwezi Agosti mwaka 2000 ni sehemu kubwa kabisa yenye mwinuko wa juu kabisa kutoka uso wa bahari ambayo ni hifadhi ya maumbile yenye viumbe wengi kabisa. Hifadhi hiyo iko kwenye Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, ambayo iko katika sehemu ya chanzo cha Mto Changjiang, Mto Manjano na Mto Lancangjiang. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2002, sehemu za aina mbalimbali za hifadhi ya maumbile zipatazo 1757 zilijengwa kote nchini China, eneo la jumla la hifadhi hizo limefikia hekta milioni 132.95, ambalo ni 13.2 % ya eneo la jumla la nchi kavu ya China. Sehemu hizo za hifadhi ya maumbile zimefanya kazi muhimu za kutunza vyanzo vya mito, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, kuzuia upepo na kuimarisha mchanga na kuboresha hali ya hewa ya kikanda; na sehemu nyingi za hifadhi ya maumbile zimekuwa sehemu muhimu ya hifadhi ya aina nyingi za viumbe duniani. Na mkoani Yunnan kuna sehemu nyingi zaidi za hifadhi ya maumbile kuliko mikoa mingine, sehemu hizo zimefikia 152 na eneo la sehemu hizo zimefikia hekta milioni 2.8. Sehemu 22 kama vile hifadhi ya maumbile za Wolong na Jiuzaigou mkoani Sichuan, Mlima Changbei mkoani Jilin, Mlima Dinshan mkoani Guangdong na Mto Beishui mkoani Gansu zimeorodheshwa na shirika la UNESCO la Umoja wa Mataifa kuwa "sehemu za hifadhi ya viumbe duniani".


1 2 3 4 5 6