12: Wanawake

Kulinda Haki na Maslahi ya Wanawake

Sheria na Kanuni za Kulinda Haki na Maslahi ya Wanawake

Hivi sasa China imeanzisha mfumo wa kisheria wa kulinda haki na maslahi ya wanawake na kuhimiza usawa kati ya wanaume na wanawake kwa msingi wa katiba. Sheria hizo ni pamoja na "sheria ya raia", "sheria ya makosa ya jinai", "sheria ya upigaji kura", "sheria ya kazi", "sheria ya ndoa", "sheria ya idadi ya watu na uzazi wa mpango", "sheria ya kusaini mkataba wa kulima mashamba" na kadhalika. Tokea "sheria ya kuhakikisha haki na maslahi ya wanawake ya Jamhuri ya Watu wa China" itolewe mwezi Aprili mwaka 1992, Bunge la Umma la China limetunga sheria 12 na maazimio mawili husika ya kulinda haki na maslahi ya wanawake, kama vile "sheria ya kazi", "sheria ya kuchagua kamati ya wanavijiji", "sheria ya kuhakikisha haki na maslahi ya wazee", "sheria ya idadi ya watu na uzazi wa mpango" na "sheria ya kusaini mkataba wa kulima mashamba".

Wakati huo huo, China pia imerekebisha sheria 7 zinazohusiana na haki na maslahi ya wanawake kama vile "sheria ya upigaji kura", "sheria ya makosa ya jinai" na "sheria ya ndoa". Baraza la serikali limetunga sheria na kanuni 7 kuhusu kulinda haki na maslahi ya wanawake, na idara nyingine husika zimetunga kanuni 98 husika. Mikoa na miji yote imechukua hatua za kutekeleza sheria hizo. Ili kuhimiza utekelezaji wa sheria hizo, idara husika na sehemu mbalimbali pia zimetunga nyaraka za sera, na kuanzisha harakati za kueneza sera hizo ili watu wote wafahamishwe jinsi ya kulinda haki na maslahi ya wanawake.

Haki ya Wanawake wa China ya Kupewa Ajira

Ili kuwahakikishia wanawake haki ya kupewa ajira, idara husika za China siku zote zinatekeleza kwa bidii "sheria ya kazi", kupiga marufuku ubaguzi wa kijinsia wakati wa kuajiri watumishi; kuwahakikishia wanawake wawe na haki ya kumiliki mali na ufundi sawa na wanaume, kuhakikisha kuwa wanaume na wanawake wanafanya kazi ya aina moja na kupata mshahara sawa, kupunguza pengo la mapato kati ya wanaume na wanawake; na kupanua maeneo ya kuwaajiri wanawake. Kukuza shughuli za utoaji huduma ili kuongeza nafasi za ajira kwa wanawake; kutekeleza vizuri sera ya kulinda kazi ya wafanyakazi wanawake, wanawake wa vijijini wana haki sawa na wanaume katika kusaini mkataba wa kulima mashamba, kuendesha uzalishaji, na kupewa ardhi ya kujenga nyumba, kuwaelekeza na kuwasaidia wanawake wa vijijini wajifunze ufundi wa kikazi ili waweze kufanya shughuli nyingine licha ya kilimo.

Haki ya Wanawake ya Kupata Elimu

"Katiba", "sheria ya kutoa elimu ya lazima", "sheria ya kuhakikisha haki na maslahi ya wanawake" na sheria nyingine za China zote zina vifungu vinavyoeleza kuwa, wanawake wana haki sawa na wanaume ya kupata elimu. Mwaka 2001, asilimia 99.1 ya watoto wa China wenye umri wa kwenda shule walipata nafasi ya kwenda shule, ambapo asilimia 99.01 ya watoto wa kike walipata nafasi ya kwenda shule, Mwaka 2002, wanafunzi wa kike walichukua asilimia 46.7 ya wanafunzi wote wa shule za sekondari, ambapo kiasi cha wanafunzi wa kike katika vyuo vikuu kilichukua asilimia 44. Katika miaka ya hivi karibuni, kiwango cha wanawake wa China cha kupata elimu kimeinuka sana, na tofauti kati ya wanaume na wanawake katika kupata elimu inapungua siku hadi siku. Kutokana na takwimu ya sensa ya 5 iliyofanyika mwaka 2000, wanawake wa China kwa wastani walipata elimu ya miaka 7.07, tofauti ya kupata elimu kati ya wanawake na wanaume ilipungua kufikia mwaka 1.07 kutoka ile ya 1.40 ya mwaka 1995.

Hakikisho la afya kwa wanawake wa China

Katika miaka ya hivi karibuni, hali ya afya ya wanawake wa China imeboreshwa kidhahiri. Ilipofika mwaka 2002, asilimia 86 ya wajawazito wa China walipewa huduma za afya, na asilimia 78.8 ya wajawazito walijifungua hospitalini, na kiasi cha wajawazito waliokufa wakati wa kujifungua kilipungua sana. Wastani wa maisha ya wanawake ni miaka 73.6, ukiwazidi wanaume kwa miaka 3.8.

China imeanzisha mtandao wa huduma za afya vijijini. Kuanzia mwaka 2000 hadi 2001, serikali kuu na serikali za mikoa zilianzisha harakati ya kupunguza vifo vya wajawazito na kutokomeza hali ya watoto wachanga kupata ugonjwa wa pepo punda katika mikoa, miji na mikoa inayojiendesha ya magharibi mwa China, kuimarisha ujenzi wa hospitali za uzazi katika vitongoji vilivyoko katika sehemu maskini, na kuwaandaa wafanyakazi wa sekta ya afya.

Mwezi Aprili mwaka 2001, baraza la serikali lilitoa "utaratibu wa kutekeleza sheria ya afya ya mama na watoto wachanga ya Jamhuri ya Watu wa China", ikidhihirisha zaidi huduma zinazopaswa kutolewa kwa wanawake na watoto, kuimarisha kazi ya kupima na kutibu maradhi ya wanawake nchini. Ilipofika mwaka 2002, vituo 3067 vya afya vya wanawake na watoto vilianzishwa nchini kote.

Serikali ya China inatilia maanani sana kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi, ikiwa imetunga "mpango wa kipindi kirefu na cha wastani wa kinga na tiba ya ukimwi"(1998-2010) na "mpango wa kuzuia na kutibu ukimwi wa China" (2001-2005). Serikali katika ngazi tofauti zinafuatilia sana kueneza ujuzi kuhusu jinsi ya kukinga ukimwi na magonjwa ya zinaa, kuzuia maambukizi kutoka kwa mama wazazi hadi kwa watoto.

Haki na maslahi sawa ya wanawake katika ndoa na familia

Kati ya familia milioni 350 za China, familia nyingi zinaundwa kutokana na ndoa halali ya kujiamulia kwa msingi wa kupendana, uhusiano kati ya wanaume na wanawake katika familia ni sawa na kusikilizana, wanawake wana uhuru na haki juu ya mali.

Mwezi Aprili mwaka 2001, Halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China ilitoa sheria mpya ya ndoa. Sheria hiyo inapiga marufuku kuwa na wake au waume wawili, ni haramu kwa mtu mwenye mke au mume kuishi pamoja na mwingine, kupiga marufuku kufanya vitendo vya kimabavu nyumbani, kuweka utaratibu kuhusu ndoa ambazo hazitambuliki, kukamilisha utaratibu wa kugawa mali za familia kati ya mume na mke, kuweka utaratibu wa kufidia hasara kutokana na talaka na vitendo vya kimabavu nyumbani, kuhukumu vitendo vya kuharibu ndoa na familia ili kulinda hadhi ya wanawake katika familia.

Ili kuanzisha uhusiano wa kindoa na kifamilia wenye usawa, masikilizano na ustaarabu, China imeunda kikundi cha kuratibu shughuli za kujenga familia bora cha China kilichoundwa pamoja na mashirika 18 ya serikali na yasiyo ya serikali, na kuzifaya shughuli za kujenga familia bora katika mpango mkuu wa maendeleo ya uchumi na ujenzi wa ustaarabu. Mwaka 2000 matokeo ya uchunguzi uliofanywa na Shirikisho Kuu la Wanawake la China na Idara ya Utoaji Takwimu ya China yalionesha kuwa, asilimia 93.2 ya wanawake wa miji na vijiji waliona kuridhika na hali yao ya ndoa.


1 2 3 4 5 6 7