Sanamu
Mpiga Mshale Aliyepiga Goti
Sanamu hiyo ina kimo cha sentimita 120, ilifukuliwa kutoka kwenye kaburi la Qinshihuang mfalme wa Enzi ya Tang mkoani Shanxi.
Hii ni sanamu ya mtu aliyefyatua mshale akiwa amepiga goti la kulia, na kuinua kifua. Ni sanamu iliyogunduliwa kati ya sanamu za askari na farasi zilizozikwa ndani ya kaburi la mfalme Qinshihuang.
Kusimulia Hadithi kwa Kupiga Ngoma
Sanamu hiyo ina kimo cha sentimita 55, ilitengenezwa katika Enzi ya Han Mashariki, na ilifukuliwa mkoani Sichuan, na sasa inahifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Taifa.
Sanamu nyingi za kale zilifukuliwa mkoani Sichuan na iliyo maarufu sana ni sanamu hiyo. Sanamu hiyo inaonesha mtu mwenye kichwa kikubwa kilichovaa kilemba na uso wenye makunyanzi tele. Ngoma ndogo kwenye mkono wa kushoto na mkono wenye kijiti juu, ikionesha msimulizi huyo akieleza hadithi yake kwa msisimko.
Chui wa Fedha
Mungu Mwanamke Guanyin Mwenye Mikono Elfu Mmoja
Ndani ya hekalu la Shuanglin kuna kumbi kubwa mbalimbali ambazo ndani yake kuna sanamu za miungu mingi, mmoja kati ya hizo ni mungu mwanamke Guanyin mwenye mikono elfu moja. Hekalu hilo lilijengwa katika Enzi ya Wei Kaskazini(386-534).
Farasi Anayekimbia juu ya Mbayuwayu
Sanamu hiyo ilitengenezwa kwa shaba nyeusi, na ina kimo cha sentimita 34.5, urefu wa sentimita 45 na upana wa sentimita 10. Ni sanamu iliyotengenezwa katika Enzi ya Han Mashariki (25-220), na ilifukuliwa mkoani Gansu, hivi sasa inahifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Mkoa wa Gansu.
Farasi walikuwa ni kama chombo muhimu vitani, na alama ya heshima ya taifa na nguvu za nchi. Sanamu za farasi za Enzi ya Han ziligunduliwa, lakini iliyoshangaza ni sanamu hiyo.
Farasi huyo anakimbia shoti kichwa juu na miguu mitatu hewani na mguu mmoja tu uko juu ya bawa la mbayuwayu. Misuli inaonesha afya na nguvu za farasi, uzito wote wa farasi uko kwenye bawa la mbayuwayu.
Farasi aliyekimbia ni sanamu adimu kati ya sanamu za kale.
Beseni la Udongo Yenye Rangi
Beseni la udongo lenye rangi iligunduliwa mwaka 1973 katika wilaya ya Datung, mkoani Qinghai. Kwenye beseni hilo kuna michoro wa wasichana wanaocheza ngoma, hadi sasa beseni hilo lina historia ya miaka 5000.
|