Mlima E Mei na Sanamu Kubwa ya Buddha
Mlima E Mei uko katikati ya kusini mkoani Sichuan, magharibi mwa China. Mlima huo una urefu wa mita 3099 kutoka usawa wa bahari.
Mlima E Mei unafunikwa na mimea mwaka mzima kutokana na sura yake ya ardhi, mvua ya kutosha na tofauti za hali ya hewa. Katika eneo lenye kilomita 100 za mraba kuna mimea ya aina zaidi ya 100 ambayo ni moja ya kumi ya mimea yote nchini China, na aina 2300 za wanyamapori.
Mlima E Mei ni moja ya "milima mikubwa minne takatifu ya dini ya Buddha". Hivi sasa kuna mahekabu yaliyobaki katika mlima huo karibu thelathini, na kubwa zaidi kati mahekalu hayo ni hekalu la Wanniansi
Katika mlima huo kuna sanamu kubwa ya Buddha. Sanamu hiyo iko mlimani Qingyijiang, sanamu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 713, na ilimalizika katika muda wa miaka 90. Kichwa cha sanamu hiyo ni sawa na kilele cha mlima, miguu inakanyaga makutano ya mito mitatu, mikono miwili inashika magoti, kimo chake ni mita 71, urefu wa kichwa ni mita 15, urefu wa sikio ni mita 7 na upana wa mabega ni mita 28. Mgongo wake unaweza kukaliwa na watu kama mia moja. Hii ni sanamu kubwa kweli na pia ni sanamu pekee iliyotengenezwa kwenye genge la mlima.
Mandhari ya Mlima E Mei na utamaduni wake wa historia ni mali adimu kwa ajili ya utafiti wa historia, na utalii, ni mali ya binadamu wote.
Mwaka 1996 Mlima E Mei na sanamu hiyo ya Buddha iliorodheshwa katika urithi wa dunia. Kamati ya Urithi wa Dunia ilitathmini kuwa mandhari ya Mlima E Mei na sanamu kubwa ya Buddha ni nzuri kweli, kutokana na historia ndefu, sehemu hiyo ni muhimu katika utamaduni wa binadamu.
|