24: Wanamuziki

Wanamuziki

Mtungaji Muziki Liu Wenjin

Bw. Liu Wenjin ni mtunzi wa muziki mashuhuri nchini, alihitimu masomo yake mwaka 1961 katika chuo cha muziki cha taifa. Aliwahi kuteuliwa kuwa kiongozi wa bendi ya taifa ya ala za muziki za jadi, msimamizi mkuu wa sanaa na mkuu wa kundi la michezo ya opera ya taifa; hivi sasa yeye ni mwongozaji wa sanaa wa kundi la michezo ya opera la taifa. Mwaka 2001 aliajiriwa kuwa profesa wa chuo kikuu cha ala za muziki za jadi cha Korea ya Kusini.

Bw. Liu Wenjin alikuwa na mafanikio mazuri aliposoma chuoni na aliwahi kupata tuzo ya "mwanafunzi hodari" iliyotolewa na chuo cha muziki cha taifa. Alitunga muziki mwingi, na ule aliotunga mwaka 1999 "Ukuta Mkuu" ulipata tuzo ya ngazi ya kwanza ya taifa.

Katika miaka zaidi ya 40 iliyopita Bw. Liu Wenjin alitunga na kurekebisha muziki na nyimbo nyingi za kijadi, na kutunga muziki kwa ajili michezo ya ngoma, opera, sinema na michezo ya televisheni. Bw. Liu Wenjin pia alishiriki kwenye utungaji wa mchezo mkubwa wa nyimbo na ngoma ijulikanayo kwa "Nyimbo za mapinduzi ya China".

Bw. Liu Wenjin amesifiwa na wanamuziki wa China kuwa ni mtunzi hodari wa muziki nchini China, mwezi Septemba mwaka 1989 bendi ya ala za muziki za jadi ya Hong Kong ilifanya maonesho ya muziki yajulikanayo kwa jina la "Toka Liu Tianhua hadi Liu Wenjin".

Taasisi ya utafiti wa muziki wa China ya Amerika ya kaskazini ijulikanayo kwa "CHINESE MUSIC" inamsifu Liu Wenjin kuwa ni mwanamuziki mkubwa wa China bara, na kuchapisha makala nyingi za maelezo kuhusu muziki wa jadi aliotunga.

Bw. Liu Wenjin alialikwa kutembelea nchi makumi kadhaa zikiwemo za Ulaya, Marekani na Asia pamoja na sehemu za Hong Kong, Macao na Taiwan za China. Yeye na wanamuziki wa Japan na Korea ya Kusini walianzisha bendi ya muziki ya Asia.

Bw. Liu Wenjin aliteuliwa na wizara ya utamaduni kuwa msanii mwenye mafanikio makubwa, alitunukiwa shahada ya heshima na kupewa kiinua mgongo maalumu na serikali.

Gao Weijie

Bw. Gao Weijie ni mtungaji muziki mashuhuri nchini ambaye alimaliza masomo katika chuo cha muziki cha Sichuan. Aliwahi kuwa mkurugenzi wa kitivo cha utungaji muziki cha chuo cha muziki cha Sichuan, mkurugenzi wa kitivo cha utungaji muziki cha chuo cha muziki cha taifa na mhariri wa jarida la "Muziki wa Umma".

Mwaka 1983 Bw. Gao Weijie alianzisha kikundi cha kwanza cha muziki wa kisasa cha China kinachojulikana kwa "Jumuiya ya utafiti wa utungaji wa wanamuziki" na kuwa kiongozi wa jumuiya hiyo. Hivi sasa Bw. Gao Weijie ni profesa wa chuo cha muziki cha taifa, msimamizi wa maalumu wa miradi ya utafiti wa idara ya utafiti wa taaluma ya muziki wa chuo cha muziki cha taifa, na kualikwa kuwa profesa wa chuo kikuu cha Yanbian na chuo kikuu kimoja nchini Marekani, na pia ni mhariri wa jarida la "Muziki wa China" na "Taaluma ya muziki wa China".

Muziki aliotunga ulipinga nchini na katika nchi za nje na alipata tuzo nyingi. Muziki aliotunga ni pamoja na orchestra ya "mambo ya zamani kwenye mbuga". Katika miaka ziaidi ya 40 Bw Gao Weijie alifundisha wanafunzi wengi ambao walipata tuzo nyingi katika mashindano ya utungaji muziki na baadhi yao wamekuwa watunga muziki mashuhuri. Bw. Gao Weijie alialikwa kutembelea New Zealand, Korea ya Kusini, Ufaransa, Uingereza, Marekani na nchi nyingine. Hivi sasa anapata kiinua mgongo maalumu kutoka kwa baraza la serikali.

Fu Lin

Bw. Fu Lin alizaliwa tarehe 17 mwezi Januari mwaka 1946, mwaka 1968 alimaliza masomo katika kitivo cha muziki cha chuo cha sanaa cha jeshi la ukombozi la umma la China, alikuwa mchezaji wa ala za muziki, naibu kiongozi na mwongozaji wa sanaa wa kikundi cha nyimbo na ngoma cha jeshi la baharini la China, vile vile alikuwa naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo ya jumuiya ya muziki ya China na kuwa naibu mwenyekiti wa jumuiya ya muziki wa kawaida ya China.

Katika miaka karibu 40 iliyopita alitunga nyimbo zaidi ya 1,000, lakini alisema kuwa hakuna wimbo aliotunga ambao unampendeza yeye mwenyewe. Alisema kuwa nyimbo wanazopenda watu ndio anazozipenda yeye.

Bw. Fu Lin alitunga muziki kwa ajili ya filamu zaidi ya 100 za sinema. Hivi sasa utungaji muziki ni moja ya kazi zake, na anatumia nafasi nyingi zaidi kufanya utafiti kuhusu nadharia ya muziki na kufundisha vijana wa muziki.

Katika mwaka 1986 na mwaka 1987 alifanya maonesho katika miji ya Haerbin na Xian, China ya nyimbo na muziki aliotunga yeye, ambayo ulioneshwa kwenye kituo cha televisheni cha CCTV mwaka 2001.

Wang Luobin

Bw. Wang Luobin (1913-1996) anasifiwa kama ni mwenezaji wa nyimbo za jadi za sehemu ya magharibi ya China na bingwa wa nyimbo za mtindo wa kisasa nchini China. Alizaliwa Beijing mwezi Januari mwaka 1913. Harakati za utamaduni mpya zilipojitokeza mwaka 1919 wakati alikuwa akisoma katika shule ya msingi, alianza kujifunza baadhi ya nyimbo za nchi za magharibi na Japan. Mwaka 1924 Bw. Wang Luobin alisoma katika sekondari ya wamisionari, alishiriki kwenye kikundi cha kwaya ambapo alifahamu sauti zinazolingana za nyimbo ( harmony ). Mwaka 1931 aliposoma katika chuo cha ualimu cha Beijing alijifunza uimbaji na kucheza piano kwa kumfuata mwalimu Bibi Horwath kutoka Urusi na kufundishwa muziki wa kijadi.

Mwaka 1937 Bw. Wang Luobin alishiriki kikundi cha sanaa kwenye medani ya sehemu ya kaskazini magharibi kilichoongozwa na mwandishi vitabu mashuhuri bibi Ding Lin. Mwaka 1938 alipata uhamisho kwenda sehemu ya Xinjiang ambapo alisikia nyimbo nyingi za kupendeza za huko, akaanza kukusanya nyimbo za makabila madogo madogo.

Baada ya hapo Bw. Wang Luobin kila mara akifika katika sehemu mpya anajitahidi kukusanya nyimbo za jadi, kutokana na juhudi zake Bw. Wang Luobin amekusanya na kurekebisha nyimbo nyingi za Xinjiang, ambazo zinapendwa na watu hadi hivi sasa.

Kutokana na msingi wa kukusanya nyimbo za jadi, Bw. Wang Luobin alirekebisha baadhi ya nyimbo ambazo zilienea katika mikoa ya Gansu na Qinghai, kisha zikaenea katika sehemu mbalimbali nchini na katika miaka makumi kadhaa iliyopita nyimbo hizo zinapendwa na wachina wengi.

Lei Zhenbang

Bw. Lei Zhenbang (1916-1997) ni mtungaji muziki wa sinema, aliwahi kuwa mratibu wa jumuiya ya wanamuziki ya China na mratibu wa jumuiya ya wacheza sinema wa China na kuwa mjumbe wa baraza la 6 la mashauriano ya kisiasa ya China. Bw. Lei Zhenbang alizaliwa mwezi Mei mwaka 1916 katika ukoo mmoja tajiri wa kabila la waman, alipenda kusikiliza opera ya Kibeijing, tangu alipokuwa na umri wa miaka 7 aliweza kuimba baadhi ya sehemu za michezo ya opera ya Kibeijing na nyimbo.

Mwezi Januari mwaka 1939 Bw. Lei Zhenbang alikwenda kusomea elimu ya muziki katika darasa la maandalizi kabla ya kuwa mwanafunzi wa chuo hicho cha muziki nchini Japan, na aliruhusiwa na mkuu wa shule kuwa mwanafunzi rasmi wa chuo cha muziki katika muda usiotimia nusu mwaka.

Bw. Lei Zhenbang alirejea nchini mwaka 1943 na kuwa mwalimu wa muziki katika sekondari ya wasichana ya Beijing na sekondari ya Huizhong mjini Beijing. Baada ya ushindi wa vita ya kupambana na mashambulizi ya Japan, alianzisha kikundi cha simphony cha baada ya masomo chenye watu zaidi ya 50.

Bw. Lei Zhenbang alirekebisha muziki wa kale wa China ujulikanao kwa "wimbo wa huzuni" kuwa muziki wa orchestra kwa ajili ya maonesho ya bendi hiyo.

Mwezi Juni mwaka 1949 Bw. Lei Zhenbang alipata uhamisho kwenda kufanya kazi ya kutunga muziki katika kiwanda cha filamu za sinema cha Changchun.

Katika muda wa miaka zaidi ya 30 baada ya hapo alitunga nyimbo zaidi ya 100 kwa ajili ya filamu za sinema zinazopendwa na watu wengi, na baadhi yao zilipata tuzo za muziki.

Katika mwaka 1960, mwaka 1964 na mwaka 1980 muziki nyingi alizotunga zilipata tuzo za tungo bora.

Katika miongo kadhaa iliyopita muziki aliotunga kwa ajili ya filamu za sinema ikiwemo "Dong Cunrui". "Dada wa tatu wa ukoo wa Liu" na "mgeni kutoka mlima wa wenye theluji" inapendwa sana na watu.

Zhang Li

Mtungaji wa maneno ya nyimbo Bw. Zhang Li alizaliwa katika mji wa Dalian tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka 1932. Mwaka 1948 alisoma kitivo cha fasihi katika chuo cha sanaa cha Lu Xun cha sehemu ya kaskazini mashariki. Mwaka 1955 alifundisha katika kitivo cha fasihi cha chuo kikuu cha ualimu cha Beijing na alihamishwa katika ofisi ya utungaji ya bendi ya ala za muziki za jadi cha taifa na kuwa mtungaji wa michezo wa ngazi ya kwanza ya taifa.

Katika miaka zaidi ya 50 iliyopita alitunga nyimbo nyingi zinazopendeza watu zikiwemo "kivuli cha fencing ", "maisha yenye furaha na uchungu" na "Upepo wa Asia" ambazo zinapendwa sana na watu.

Bw. Hang Li alipita kwenye njia yenye shida nyingi hadi kufikia kwenye mafanikio. Katika miaka ya 60 ya karne ya 20 nyimbo alizotunga hazikupendwa na baadhi ya wataalamu na wanamuziki, lakini hakufa moyo, bali alijitahidi zaidi kuliko zamani, hatimaye alifanikiwa.

Hivi sasa ingawa amekuwa na umri wa miaka zaidi ya 70, na afya zake si nzuri sana, lakini bado ana shughuli nyingi, anaendelea kufanya kazi za utungaji, kushiriki katika semina na shughuli za kufundisha utungaji wa maneno ya nyimbo.

Tian Han

Tian Han ni mmoja ya watu waliojijengea msingi wa harakati za michezo ya kuigiza nchini China, na ni mtangulizi wa mageuzi ya michezo ya opera. Si kama tu alitunga michezo ya kuigiza na opera, bali alitunga michezo ya sinema, mashairi na nyimbo za sinema.

Bw. Tian Han alizaliwa tarehe 12 mwezi Machi mwaka 1898 katika ukoo wa wakulima mkoani Hunan. Bw. Tian Han alishiriki harakati za utamaduni mpya za kupinga ubeberu na umwinyi toka "vuguvugu la tarehe 4 Mei". Alijiunga na chama cha kikomunisti cha China mwaka 1932, na baada ya hapo aliingia katika kipindi cha pili cha utungaji. Bw. Tian Han alitunga maneno ya wimbo wa jeshi la kujitolea ambao uliwahamasisha wachina wengi kushiriki kwenye vita ya kupambana na mashambulizi ya Japan na kulikomboa taifa, wimbo huo ulifanywa kuwa wimbo wa taifa baada ya kuasisiwa kwa China mpya.

Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, Bw. Tian Han alikuwa kiongozi kwenye kazi yake, lakini hakuacha kazi ya utungaji. Mchezo wa historia aliotunga ujulikanao kwa "Guan Hanqing" ulionesha heshima yake kwa mtu huyo wa kale ambaye alimlalamikia Dou Er ambaye aliadhibiwa kwa makosa na kutendewa isivyo vya haki, lakini yeye mwenyewe aliteswa hadi kufariki dunia na "genge la watu wanne". Mwaka 1968 aliugua ugonjwa na kupotea kutokana na kuteswa siku hadi siku.

Bw. Tian Han alitunga michezo ya kuigiza zaidi ya 60, michezo ya opera zaidi ya 20, sinema zaidi ya 10, mashairi zaidi ya 900 pamoja na insha na nyimbo nyingi.

Xu Peidong

Xu Peidong (1954--- ) mtungaji muziki mashuhuri wa China.

Bw. Xu Peidong alizaliwa katika mji wa Dalian tarehe 1 mwezi Februali mwaka 1954. mwaka 1970 alifaulu mtihani wa kuingia katika kikundi cha nyimbo na ngoma cha eneo la jeshi la Fuzhou na kuwa mpiga fidla kubwa wa kwanza, mwelekezaji wa bendi na mtunga muziki. Mwaka 1985 alikuwa mtunga muziki wa ngazi ya kwanza na naibu mwenyekiti wa jumuiya ya muziki mwepesi ya China. Mwaka 1992 na mwaka 1996 aliteuliwa kuwa mmoja wa watungaji muziki wa China, na mwaka 1996 alipata "tuzo ya mafanikio ya utungaji muziki katika miaka 20" pamoja na "tuzo ya mafanikio ya utungaji wa nyimbo za mtindo wa kisasa za China".

Alitunga muziki mwingi ikiwemo ya opera za "Hisia za jenerali", "Maua ya mitende" na sinema ijulikanayo kwa "Vijana wa rock'n'roll" pamoja na muziki wa nyimbo nyingi zikiwa ni pamoja na "Mwezi wa tarehe 15 unapevuka zaidi tarehe 16".

Qiao Yu

Bw. Qiao Yu (1927---) mtungaji mashuhuri wa maneno ya nyimbo. Bw. Qiao Yu alizaliwa mwaka 1927 katika mji wa Jining mkoani Shandong ambaye anasifiwa kuwa ni bingwa wa utungaji wa maneno ya nyimbo nchini China. Mwaka 1946 alisoma katika chuo cha sanaa cha kaskazini mwa China. Aliwahi kuwa mtungaji wa opera tatu wa chuo hicho.

Baada ya China mpya kuasisiwa mwaka 1949, aliwahi kuwa mtungaji wa maneno ya nyimbo wa chuo cha michezo ya opera ya taifa, jumuiya ya watungaji wa michezo ya opera ya China na wa wizara ya utamaduni. Toka mwaka 1977 aliteuliwa kuwa naibu kiongozi na kiongozi wa kundi la michezo ya opera na ngoma la China, mratibu wa kituo cha kimataifa maingiliano ya utamaduni cha China. Alikuwa mjumbe wa baraza la 8 na mashauriano ya kisiasa la China.

Utungaji wa Bw. Qiao Yu unaendana na wakati, katika miaka ya 50 ya karne iliyopita alitunga michezo ya fasihi ya sinema ya "binti wa tatu wa ukoo wa Liu", "Watoto Wekundu" maneno ya wimbo wa "Nchi Yangu". Baada ya kuigia katika miaka ya 80, wakati ambapo China ilianza kutekeleza sera ya mageuzi, Bw. Qiao Yu alitunga maneno ya nyimbo nyingi zikiwemo za "Waridi wa moyoni mwangu", "Usiku wa leo usiosahaulika" pamoja na nyingi nyinginezo, ambazo zinapendwa na watu wengi.

Tungo nzuri zaidi za Bw. Qiao Yu ni pamoja na "Nchi Yangu", "watu wanasifu mandhari nzuri ya Shanxi" na "waridi wa moyoni mwangu".

Nie Er

Bw. Nie Er (1912---1935) mtunga mashuhuri wa muziki wa China.

Bw. Nie Er alizaliwa tarehe 14 mwezi Februali mwaka 1912 katika mji wa Kunming mkoani Yunnan, China. Mwaka 1918 alisoma katika shule ya msingi ya chuo cha ualimu cha Kunming. Alipata mafanikio mazuri katika masomo yake na alipenda sana muziki. Baada ya masomo alijifunza kupiga ala za muziki za jadi zikiwa ni filimbi, zeze la kichina na gambusi, hivyo anafahamu sana muziki ya jadi. Mwaka 1927 alifaulu mtihani na kusoma katika chuo cha kwanza cha ualimu mkoani Yunnan na kuanzisha "jumuiya ya muziki ya tisatisa" na kuanza kufanya maonesho chuoni na sehemu za nje, wakati ule alianza kujifunza fidla ya nchi za magharibi na piano.

Mwezi Novemba mwaka 1930 Bw. Nie Er alijiunga na "Umoja wa kupinga ubeberu". Mwezi Machi mwaka 1931 alikuwa mpiga fidla katika kikundi cha opera cha Mingyue. Mwezi Aprili mwaka 1932 alifahamiana na mtungaji wa michezo ya opera na mshairi Bw. Tian Han, kutokana na kuathiriwa naye Bw. Nie Er alikwenda Beijing mwezi Agosti mwaka 1932 na kujiunga na umoja wa wanamuziki wa mrengo wa kushoto, na kujifunza kupiga fidla kutoka mwalimu wa kigeni Bw. Tonov. Alirejea mjini Shanghai mwezi Novemba.

Baada ya kurejea Shanghai Bw. Nie Er alifanya kazi katika kampuni ya filamu za sinema ya Lianhua na alijitahidi kushiriki katika harakati za muziki, opera na sinema za mrengo wa kushoto. Aidha alishiriki katika shughuli za muziki za "Jumuiya ya marafiki wa Urusi" na kuanzisha "Jumuiya ya utafiti wa muziki ya Xinxing".

Mwaka 1933 Bw. Nie Er alitunga muziki mpya wa mtindo mpya kabisa ukiwemo ya "Wimbo wa uchimbaji madini" na "Wimbo wa uuzaji wa magazeti". Mwaka 1934 alitengenezesha sahani za santuri za "Wimbo wa barabara kubwa", "Watangulizi" na "Wimbo wa kuhitimu masomo". Mwaka 1935 alitunga muziki wa nyimbo za "Muziki wa Meiniang", "Wasichana wa vijijini" na "Wimbo wa kusonga mbele wa jeshi la kujitolea" ambao ulikuwa wimbo wa taifa baada ya kuasisiwa China mpya.

Tarehe 18 mwezi Aprili mwaka 1935 Bw. Nie Er aliwasili Tokyo, Japan ambapo alifanya uchunguzi kuhusu muziki, michezo ya opera na sinema, aliwafahamisha sekta ya fasihi na sanaa ya Japan kuhusu maendeleo mapya ya muziki nchini China, na alijifunza lugha na muziki wa Japan. Bw. Nie Er alifariki katika maji nchini Japan tarehe 17 mwezi Julai alipokuwa na umri wa miaka 23 tu.

Bw. Nie Er alikuwa na muda wa miaka kiasi cha miwili ya kutunga muziki, lakini alitunga muziki wa aina 20 hivi kwa ajili ya nyimbo za filamu 8 za sinema, michezo mitatu ya kuigiza na opera moja. Licha ya hayo alitunga muziki wa aina 41 ukiwa ni pamoja na nyimbo 15 na muziki wa aina nne wa ala za jadi. ?

Liu Tianhua

Bw. Liu Tianhua (1895---1932) alikuwa mtungaji muziki mashuhuri, mwanamuziki na mwalimu wa ala za muziki za jadi. Bw. Liu Tianhua alizaliwa mwaka 1895 katika ukoo wa msomi wa wilaya ya Jiangyin, mkoani Jiangsu. Ndugu watatu wa ukoo huo wote ni hodari. Mwaka 1912 Bw. Liu Tianhua alishiriki kwenye bendi moja mjini Shanghai, na kujifunza nadharia ya muziki, piano, fidla na za aina nyingine. Alirejea kwao mwaka 1914 na kufundisha masomo ya muziki katika shule moja ya sekondari.

Mwaka 1915 Bw. Liu Tianhua alifiwa na baba yake, ambapo katika majonzi makubwa alitunga muziki "kupiga kite", na kuanza kushika njia ya utungaji wa muziki.

Ili kujifunza muziki ya jadi ya China Bw. Liu Tianhua aliwatembelea wanamuziki wa jadi na kujifunza kutumia ala za muziki za kijadi. Alifanya mageuzi kuhusu upigaji wa zeze la kijadi na kufanya upigaji wa ala hiyo ya muziki kuoneshwa katika maonesho ya muziki na kufundishwa katika vyuo vya muziki.

Katika miaka 10 ya kutoka mwaka 1922 hadi 1932, Bw. Liu Tianhua alikuwa profesa wa ala za muziki za zeze ya kijadi, gambusi na fidla. Katika utungaji wa muziki alirithi ufundi wa utungaji wa muziki wa kijadi huku akijifunza mbinu ya utungaji wa muziki ya nchi za magharibi.

Toka alipokuwa na umri wa miaka 17 Bw. Liu Tianhua alianza kufundisha muziki katika shule za msingi na sekondari, na alikuwa na uzoefu mwingi wa kufundisha, na aliweka msingi wa mfumo wa elimu ya muziki wa kijadi.

Alipoanza kuwa na mafanikio makubwa Bw. Liu Tianhua alianza kuugua, mwezi Mei mwaka 1932. Wakati alipofariki alikuwa na umri wa miaka 38 tu.

Muziki safi aliotunga Bw. Liu Tianhua ni pamoja na "Kupiga kite", "wimbo wa majonzi" na "Usiku mwema".


1 2 3 4 5