21: Uchoraji wa Jadi

Vitu vya nyumbani

Vyombo vya Kauri (1)

Sehemu ya Zibo mkoani Shandong ilikuwa kituo muhimu cha kutengeneza vyombo vya kauri katika historia ya China.

Samaki na sahani ya kuwekea samaki ni vitu maarufu vilivyotengenezwa huko Zibo. Mapambo kwenye sahani yalichorwa kwa mikono. Nchini China picha ya samaki inamanisha maisha marefu na kuzaa watoto wengi. Samaki kwenye sahani huchorwa kama wa kweli kwa sura na rangi.

Magamba ya samani ni sanaa ya mikono, yalichorwa kwa makini sana, baadhi magamba huchorwa kwa mistari na baadhi yanachorwa kwa rangi nyekundu giza.

Pichani, samaki anaonekana kama wa kweli ndani ya maji na amechorwa kwa mchoro mmoja bila kuchora chora.

Vyombo vya Kauri (2)

Katika China ya kale, kulikuwapo na mto wa kulalia wa kauri. Mto huo alikuwa anapewa binti anayeolewa na kwenye mto huo huchongwa maneno "mto wa kulalia wa maisha marefu".

Pichani ni mto wa kulalia kwa sura ya kichwa cha paka, mto kama huo hutumika zaidi katika mikoa ya Hebei na Shandong, kaskazini mwa China.

Vyombo vya Kauri (3)

Pichani ni watu wawili katika opera fulani, mmoja ni ofisa wa utamaduni, mwingine ni ofisa wa kijeshi. Ofisa wa utamaduni ameshika kipepeo kwa mkono mmoja na kushika ndevu kwa mkono mwingine. Ofisa wa kijeshi ameshika ndevu kwa mkono mmoja, na kuinua mguu mmoja, na upanga ameuchomeka mgongoni.

Vyombo vya Kauri (4)

Vyombo vya Kauri Vyenye Michoro ya Rangi ya Buluu vilikuwa maarufu katika Enzi ya Yuan (1206-1368).

Katika enzi hiyo kulikuwa na matanuri mengi ya kuchomea vyombo hivyo. Vyombo vya kauri vilivyochomwa vizuri vilikuwa hutolewa kwa ajili ya wafalme, na vilikuwa havikuchomwa vizuri huuzwa miongoni mwa raia. Katika enzi hiyo matanuri yalitapakaa karibu kila mahali nchini China. Michoro kwenye vyombo vya kauri ni ya aina nyingi. Baadhi inaonesha mandhari ya mito na milima, mila na desturi, maua na ndege, matunda na mboga na watu katika riwaya.

Pichani, ni bakuli lenye michoro ya buluu. Katikati ya bakuli ni mtu mwenye upanga aliyepanda farasi, ingawa picha hiyo imechorwa kwa mistari michache lakini inaonekana kama ya kweli.

Vyombo vya Kauri (5)

Vyombo vya kauri vilivyotengenezwa katika sehemu ya Zibo mkoani Shandong ni maarufu sana hasa kwa mabeseni, mitungi, bilauri.

Mitungi iliyotengenezwa katika sehemu ya Yimeng mkoani Shandong ina michoro ya samaki, na ina vishikizo pembeni, kifuniko ni kama sahani iliyofudikizwa. Picha kwenye mitungi hiyo hueleza maisha ya kawaida na huchorwa kwa mistari michache.

Vyombo vya Kauri (6)

Bilauri ni aina moya ya vyombo vya kauri katika China ya kale. Picha ya buluu huchorwa kwenye pande zote. Bilauri kama hiyo inawavutia sana wakusanyaji wa vyombo vya kale.

Pichani, bilauri lenye picha za rangi ya buluu linavutia kwa picha na umbo lake. Picha za watu waliochorwa kwenye bilauri hilo walichorwa kwa makini, ni watu wanaosimuliwa kwenye hadithi.

Vyombo vya Kauri (7)

Chupa ya kuwekea pombe. Hii ni kauri iliyopakwa rangi nyeusi ambayo onaonekana laini na ni rahisi kusafishwa. Pichani, ni chupa yenye ujazo wa pombe lita mbili na nusu. Kwenye chupa kuna maneno "lita mbili na nusu", na pembeni kuna vishikizo viwili ili kutundikwa.

Vyombo vya Kauri (8)

Katika historia ndefu ya China vyombo vya kauri vilikuwa vingi, na kati ya hivyo baadhi ni adimu sana. Pichani, chupa ya pombe iliyotengenezwa mkoani Hebei. Umbo la chupa hiyo lilitengenezwa sana katika enzi za Song na Yuan (karne ya 10-14) na enzi za Ming na Qing (karne ya 14-19).

Chupa hiyo ina shingo nyembamba na tumbo la duara. Umbo hilo hata likibadilishwa kidogo litapoteza uzuri wake. Mdomo umesanifiwa kwa kurahisisha kumimina pombe, umbo la chupa hiyo halina tofauti la la chupa iliyohifadhiwa ndani ya kasri la kifalme mjini Beijing.

Vyombo vya Kauri (9)

Katika Enzi ya Shang (1600 K.K.-1046 K.K.) aina moja ya joka lililosemekana kuwa ni mnyama mwenye uroho ilikuwa ikichorwa kwenye sahani ya shaba nyeusi. Katika enzi za Yuan, Ming na Qing (karne ya 13-19) sura ya joka hilo ilikuwa ikichorwa sana katika sahani za kauri.

Pichani ni sura ya joka hilo kwenye sahani. Joka hilo linaonekana linaruka angani katika sehemu ya katikati ya sahani na sehemu nyingine ilichorwa majani.

Jumba la Ghorofa la Udongo Kusini mwa China

Jumba la ghorofa la udongo ni makazi kwa watu wa sehemu ya kusini katika mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China. Jumba la ghorofa hujengwa kwa duara, ukuta wa jumba hilo huwa na unene wa mita moja hivi kwa udongo ulioshindiliwa, na jumba linakuwa na ghorofa mbili hadi nne. Jumba hilo limejengwa kwa duara, na katikati kuna kisima. Jumba hilo halina madirisha kwa nje. Kwenye ghorofa ya chini na ya kwanza hutumika kama ni ghala.

Watu wanaokaa katika jumba hilo ni wa ukoo mmoja. Wanaishi kwa pamoja katika jumba kama hilo kunasaidia kuimarisha uhusiano wao wa kijamaa.

Furemu ya Kuwekea Beseni ya Kunawia Uso

Furemu ya kuwekea beseni ya kunawa uso ina miguu mitatu, miguu miwili ni mirefu ili kutundikia taulo.

Pichani, miguu miwili kati ya mitatu ilirefushwa ili kutundika taulo, pande mbili za kijiti cha kutundikia taulo zimechongwa kwa sanamu. Sanammu kwenye pande mbili zinaonesha matumaini ya kupata watoto wengi.

Kabati za Samani ya Kale

Kabati ya aina ya kale ni samani ya kuwekea nguo, ndani yake kuna visehemu vidogo. Pia kuna kabati ndogo inayowekwa karibu na kitanda. Kabati hizo baadhi zinatengenezwa kwa duara, baadhi zinatengenezwa kwa umbo la mstatili, na baadhi zinatengenezwa kama masanduku ya kawaida.

Pichani ni aina moja ya kabati iliyovutia zadi matajiri katika Enzi ya Ming (1368-1644).

Tumbi ya Samaki

Pichani ni tumbi iliyofumwa kwa mwanzi, ambayo watu wa sehemu ya kusini ya China ni hodari wa kufuma tumbi za aina mbalimbali. Baadhi tumbi hizo zinafumwa kwa umbo la binadamu, baadhi zinafumwa kwa umbo la 米 na baadhi zinafumwa kwa umbo la mraba.

Nyumba ya Tajiri Wang

Katika enzi ya Ming na Qing (1368-1911), wafanyabiashara matajiri katika mkoa wa Shanxi walijitahidi kujenga nyumba zao, na baadhi bado zipo mpaka sasa.

Nyumba ya Tajiri Wang katika wilaya ya Lingshi ni moja kati ya nyumba hizo zilizojengwa katika enzi hizo.

Eneo la nyumba hiyo ina mita za mraba elfu 10, ndani yake imegawanyika katika sehemu nyingi za kuishi kwa mujibu wa hadhi ya jamaa wa ukoo. Nyumba ndani ya ua zinagawanyika nyumba kwa wanawake na kwa wanaume, na ndani ya ua kuna milango kadhaa ya nje na ya ndani na nyumba zote zinaunganishwa kwa ujia wenye paa.

Pichani ni nyumba hiyo kwa mbali, milango, ujia wenye paa na kuta zaonekana wazi.

Sanamu ya Paka juu ya Paa la Nyumba

Watu wa China wanatilia maanani kuweka mapambo juu ya paa la nyumba. Katika Enzi ya Han (206 K.K.-220 K.K.) kwenye pande mbili za mgongo wa paa huwekwa sanamu ya nyangumi. Watu walifikiri kuwa, kwa sababu nyangumi hupuliza maji, wakiwa kwenye mgongo wa paa na kupuliza maji ajali ya moto haitatokea. Lakini baadaye sanamu zilitumika, licha ya nyangumi, samaki na wanyama wengine ambao wanaoashiria baraka pia walitumika.

Pichani ni sanamu ya paka juu ya paa la nyumba mkoani Yunnan, sura ya paka huyo ilitiwa chumvi, kwamba mdomo mkubwa wazi, macho yaliyojitokeza. Sanamu hiyo imeunganishwa kwenye kigae cha nusu duara.

Vyombo vya Kuumba Maumbo ya Chakula

Tokea enzi ya Ming na Qing, vyakula vya unga vilikuwa vinatengenezwa kuwa maumbo kwa vyombo maalumu. Vyombo hivyo vilikuwa vinatengenezwa maumbo ya maua au maneno kwa ndani na kutia unga wa ngano ndani na baada ya kupikwa kwa mvuke, vyakula huwa na maumbo maalumu yenye michongo ya maua au maneno.

Pichani ni chakula chenye maneno ya "baraka", "maisha marefu" kwa umbo la pichi na majani yake. Watu hasa wazee wanaposherehekea sikukuu zao za kuzaliwa hula mikate yenye maneno kama hayo ya baraka.

Nyumba ya Tajiri Qiao Mkoani Shanxi

Mkoa wa Shanxi ni moja ya vyanzo vya utamaduni wa kale nchini China, majengo ya nyumba ni sehemu ya utamaduni huo.

Nyumba hiyo ilijengwa katika Enzi ya Qing, mpangilio wa majengo ni neno la Kichina ambalo lina maana ya "furaha mbili". Ukuta wa ua wa nyumba hiyo una kimo cha mita zaidi ya 10, ndani ya nyumba kuna nyua 19 na vyumba zaidi ya 300.

Pichani ni sanamu za kuchongwa kwenye ujia zikiwa ni pamoja na mbao zenye maandishi, mlango, nyumba hiyo inaonekana ni ya kiutamaduni sana.

Kipande cha Ukuta Mbele ya Hekalu Mkoani Shanxi

Ili kuficha hali ya ndani, mbele ya nyumba hujengwa kipande cha ukuta. Kipande cha ukuta mbele ya nyumba ya tajiri mmoja wa biashara kina uzuri wake maalumu kwa mapambo yake ukutani.

Pichani kipande cha ukuta mbele ya hekalu la Wenmiao kimepambwa kwa kuchonga dragoni. Ukuta huo una kimo cha mita 7 na urefu 10. kwenye ukuta kuna dragoni wanaocheza mawimbi. Picha hiyo inaonesha nguvu za dragoni.

Mahati

Mahati ni chombo cha seremala kwa ajili ya kupiga mstari. Uzi unapovutwa unapita sehemu ya wino na seremala hunyoosha uzi huo kupiga mstari kwenye mbao wanayotaka kukata kwa msumeno.

Mahati zilikuwa na maumbo ya aina mbalimbal;i kama vile umbo la samaki, umbo la pichi na maumbo mengine. Pichani ni mahati yenye sura ya simba.

Kitanda cha Kale

Kitanda cha kale cha China kimekuwa na historia ndefu, kitanda kimoja cha Kipindi cha Madola Yaliyopigana (karne ya 5 hadi ya 3 K.K.) kilifukuliwa, na kitanda kingine kilichokuwa katika Enzi ya Han (206 K.K.- 220 K.K.). Katika Enzi ya Song (960-1279) kilitokea kitanda chenye ukingo pembeni, na kitanda chenye ukingo katika pande tatu kilitokea katika enzi za Ming na Qing.

Pichani ni kitanda cha mwanzi, ambacho kinafaa kwa kulala, na kukaa. Kwa kupangusa pangusa kwa vitambaa, rangi nyekundu ya kitanda hicho huonekana ya kuvutia zaidi.


1 2 3 4 5 6