somo 1 salamu

 ongea na CRI
 

 • Hujambo?
  Katika Kichina kuna njia nyingi za kusalimiana. Mara kwa mara watu husema: Ni hao. Ni, wewe; hao, nzuri, Ni hao, maana yake ya Kichina ni habari gani? Unaweza kusema ní hăo wakati wowote, mahali popote na mtu mwingine.Unaweza kusema ní hăo kwa mtu usiomfahamu au mtu unaomfahamu sana. Kusema ní hăo ni kama kusema "hi" kwa Kiingereza. Kwa mfano, nikisema "ní hăo", unaweza kujibu "ní hăo" pia.
  matamshi:
  Unaweza kutumia herufi za Kiswahili kwa kukumbuka neno ní hăo.


 • Wewe unaitwa nani?
  Ukitaka kujua jina la mtu mwingine,unaweza kumwuliza kwa Kichina: nǐ jiào shén me míngzi?
  nǐ: wewe; jiào: -itwa; shén me: nini; míngzi: jina——Unaitwa nani? nǐ jiào shén me míngzi?
  Kama mwingine akikuuliza unaitwa nani, Kwanza ungejibu "wŏ jiào" "Mimi naitwa…" halafu kusema jina lako, au ujibu moja kwa moja jina lako.

 • Hii ni kadi yangu.
  Hivi sasa nchini China watu wanapokutana kwa mara ya kwanza, hupenda kubadilishana kadi za majina.Unapompa mwingine kadi hiyo, unaweza kumwambia: zhè shì wǒ de míng piàn.
  zhè: hii.
  shì: ni.
  wǒ de: yangu.
  zhè shì wǒ de: hii ni yangu.
  míng piàn: kadi.
  zhè shì wǒ de míng piàn.Hii ni kadi yangu.

 • Hatujaonana siku nyingi!
  Kama wewe na rafiki yako hamjakutana kwa siku nyingi, unaweza kusalimiana naye na kusema kwa Kichina "hǎo jiǔ bú jiàn". Hǎo jiǔ: muda mrefu; bú: kutokutana; jiàn: kuonana.