somo 11 zungumzia kuhusu unalopenda

 ongea na CRI
 

Wachina husema "kuhitaji heshima kwa binadamu ni kama kuhitaji gamba kwa mti", inamaanisha kuwa binadamu huona aibu.Wachina wengi wanatilia maanani "Mian zi". Suala la "Mian zi" inahusiana na heshima na siri ya mtu mmoja. Nchi yetu inaathiriwa na utamaduni wa Confucius kwa muda mrefu. Na fikra ya Confucius inashikilia kanuni ya masikilizano ya uhusiano kati ya watu. Hivyo "kuhifadhi sura ya watu wengine" ni njia muhimu ya kuhifadhi uhusiano baina ya watu. Aidha, fikra ya Confucius inasisitiza kuwa marafiki wanapaswa kuishi na kufa pamoja. Kama rafiki akifanya kosa, siyo vizuri kumfahamisha ana kwa ana. Kuhifadhi heshima ya mtu mwingine ni kumheshimu. Hivyo, ukumbuke kuwa ukiwa na rafiki wa kichina, uzingatie kumhifadhi sura yake.