somo 12 katika mkahawa wa chakula cha haraka

 ongea na CRI
 

Vyakula vya haraka vya kichina vinachelewesha kutokea vikilinganishwa na vyakula vya haraka vya nchi za magharibi.Baada ya mkahawa wa vyakula vya haraka la Marekani KFC kuingia kwenye soko la China mwezi Aprili mwaka 1987, vyakula vya haraka vikaingia nchini China. Huenda ni kwa sababu mazoea ya kula ya wachina ni tofauti na wale wazungu.Wachina wanapenda kuagiza vyakula vyingi,na watu wengi wanakaa kwenye meza moja na kula pamoja.
Hivi sasa, unaweza kuona KFC na McDonald's katika sehemu mbalimbali nchini China. Pia unaweza kuona aina mbalimbali za mikahawa ya vyakula vya haraka vya kichina. Mikahawa hiyo inatoa urahisi mwingi kwa watu wenye maisha ya mwendo wa haraka wa kisasa.