-
Tafadhali subirini kidogo.
Mjini Beijing kuna mikahawa mingi ya mapishi tofauti, ambapo unaweza kupata vyakula vya sehemu mbalimbali za China, hivyo wakati wa kula chakula watu huwa wanatakiwa kusubiri, na wanaposubiri wahudumu huwa wanawaambia: Qing ni men deng yi hui er, Tafadhali subirini kidogo.
qing, tafadhali,
ni men, ninyi,
deng,, kusubiri,
yi hui er, muda kidogo.
-
Tunatakiwa kusubiri kwa muda gani?
Wo men, sisi,
yao, kutakiwa,
deng,, kusubiri,
duo jiu, muda gani.
-
Unaonaje ladha ya chakula?
Wei dao, ladha,
zen me yang, namna gani.
-
Ladha ni nzuri kweli.
Zhen de, kweli,
hen, sana,
hao chi, ladha nzuri.
-
Nimeshiba.
Wachina ni watu wakarimu, wakati ukishiba unataka kuwashukuru na kuwaambia wasikupe chakula tena, unaweza kuwaambia kwa Kichina: wo chi bao le.
wo, mimi,
chi, kula,
bao, kushiba,
Le, kisaidizi cha neno.