somo 14 katika kaunta ya kuuzia vyakula au vinywaji

 ongea na CRI
 

Wachina hutumia chai na kahawa kufahamisha utamaduni wa China na wa Magharibi. Chai inawakilisha utamaduni wa nchi za mashariki, na kahawa inawakilisha utamaduni wa nchi za Magharibi. Kuanzia maelfu ya miaka iliyopita, chai imekuwa kinywaji kinachopendwa na wachina. Kutokana na hali ya hewa ya sehemu za kusini na mashariki mwa China kufaa sana kwa kilimo cha chai, hivyo sehemu hizo zinazalisha majani ya chai ya aina nyingi, na majani hayo ya chai yanauzwa nchi za nje, ambapo utamaduni wa chai wa China unaenea pia. Na neno chai katika lugha za nchi nyingi duniani linatokana na matamshi ya neno chai la Kichina, “cha”.