somo 15 kununua chakula mtaani

 ongea na CRI
 

  • Mnapenda kula chakula cha pilipili?
    Katika mikoa ya Sichuan, Hunan na sehemu nyingine nchini China, watu wanapenda kula chakula chenye pilipili, na siku hizi wasichana wengi pia wanapenda kula chakula chenye pilipili, ukienda kwenye mkahawa pamoja na marafiki zako, kwanza unaweza kuwauliza: Ni men xi huan chi la de ma? Mnapenda kula chakula cha pilipili?
    Ni men, ninyi,
    xi huan, kupenda,
    chi, kula,
    la de, cha pilipili,
    ma, kisaidizi cha neno kwa kuuliza.

  • Napenda kula mshikaki wa nyama ya kondoo
    usiku wa majira ya joto, wachina wanapenda kula mshikaki wa nyama ya kondoo na marafiki zao. Wakati huo unaweza kusema : wo xi huan chi yang rou chuan.
    wo, mimi,
    xihuan, kupenda,
    chi, kula,
    yang rou, nyama ya kondoo,
    chuan, mshikaki,
    yang rou chuan, mshikaki wa nyama ya kondoo.

  • Ndani ya chakula hiki ni nini?
    kama unataka kujua chakula fulani cha kichina kama Jiaozi , ambacho umbo lake ni kama sambusa, ndani kuna nini, unaweza kuuliza: zhe li mian shi shen me?
    zhe, hiki,
    li mian, ndani,
    shi, ni,
    shen me, nini.

  • Twende tukanunue vinywaji.
    kama ukiona kiu kweli, unaweza kumwambia rafiki yako mchina: wo men qu mai dian yin liao ba: Twende tukanunue vinywaji.
    wo men, sisi,
    qu, kwenda,
    mai, kununua,
    Dian, chache,
    yin liao, vinywaji,
    ba, kisaidizi cha maneno.