Kuhusu vijiti vya kulia vya kichina na vijiko, baadhi ya watu wanaona kuwa, China ni nchi ya kilimo, vyakula vikuu vya China ni nafaka na mboga, hivyo watu wanatumia vijiti kula chakula. Na nchi za magharibi nyingi zilikuwa ni nchi za kufuga mifugo, vyakula vikuu vyao ni vya nyama, hivyo wanapendelea kutumia vijiko. Mbali na hayo, wachina wa familia moja hula vyakula pamoja, ambapo vitoweo huwekwa kwenye sahani moja moja kwenye meza moja, hivyo watu wanatumia vijiti vya kulia kuchukua kitoweo kila mara. Na kwa wazungu, kila mtu ale vyakula vyake kwenye sahani yake. Jambo linalosisitizwa ni kuwa, ni mwiko kwa wachina kupachika vijiti vya kulia kwenye wali au kupiga bakuli kwa vijiti vya kulia.